Chelsea wanaripotiwa kuwa wapewanafasi ya kumsajili winga wa Real Madrid, Eden Hazard, ikiwa ni miaka miwili tu baada ya kuondoka Stamford Bridge kwenda Bernabeu.

Baada ya mafanikio ya miaka saba huko London Magharibi, Hazard aliruhusiwa kuondoka kwa The Blues kwa ada ya pauni milioni 89.

Mfululizo wa majeraha kule Hispania umemzuia mchezaji huyo wa kimataifa wa Ubelgiji kuwika kwa kiwango kile kile kama alipokuwa Chelsea, huku hatma yake ya Real Madrid ikiwa na walakini.

Kwea mujibu wa AS, mawakala wameiambia Chelsea kuwa wako huru kujadili uwezekano wa kuungana tena na nyota wao wa zamani.

Lakini, ripoti inadai kwamba uhamisho hauwezekani kukubaliwa, ukizingatia Chelsea bado wanadaiwa pesa na Real kwa makubaliano ambayo yalikamilishwa mnamo 2019.

Mabingwa wa Uropa pia wanakusudia kutenga sehemu kubwa ya pesa za uhamisho wa majira ya joto kwa ajili ya kumsajili mshambuliaji wa Borussia Dortmund Erling Braut Haaland.


FURAHIA KASINO MTANDAONI HUKU UKITENGEZA MKWANJA!!

Kasino ya Mayan Eagle inakukufanya kuwa bingwa wakati wowote unapoamua kuicheza. Utaburudika huku ukiendelea kutengeza mkwanja mrefu, jiunge sasa na uwe miongoni mwa mabingwa!!

tetesi, Tetesi za Soka Barani Ulaya., Meridianbet

CHEZA HAPA

ONI MOJA

  1. Hazard ameshindwa kuwika kabisa ndani ya Madrid, Nadhani si wakati sahihi kurudi Chelsea kama bado nafasi yake ipo ndani ya Madrid

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa