Chelsea wanaripotiwa kupata kikwazo kwenye mpango wa kumsajili nyota wa Inter milan, Romelu Lukaku.

Chelsea, ambao walitwaa ubingwa wa Ulaya mwezi Mei, wana uwezo wa kifedha wa kuinasa saini ya fowadi huyo wa Inter Milan.

Licha ya Erling Braut Haaland kutajwa kama kipaumbele cha Chelsea kwa sasa kwenye dirisha la uhamisho, kuna taarifa kuwa atayari wameshaangalia uwezekano wa kuungana tena na Lukaku.

Romelu Lukaku

Hata hivyo, kwa mujibu wa Tuttosport, Inter Milan hawajajiandaa kuachana na staa wao mwenye nafasi muhimu kwa sasa klabuni hapo, angalau wanaweza kuzingatia ofa ambayo si chini ya £102.5m.

Licha ya kuwa vyema na rekodi zao za kifedha, Inter wanaamini Lukaku ana thamani kubwa na hapaswi kushikika linapokuja suala la kumuondoa klabuni hapo.

Lukaku ambaye ametumia kipindi kirefu cha maisha yake ya soka kwenye Ligi Kuu Uingereza, anawapa changamoto Chelsea kufanya maamuzi magumu au kuachana na dili hilo.


FURAHIA KASINO MTANDAONI HUKU UKITENGEZA MKWANJA!!

Kasino ya Mayan Eagle inakukufanya kuwa bingwa wakati wowote unapoamua kuicheza. Utaburudika huku ukiendelea kutengeza mkwanja mrefu, jiunge sasa na uwe miongoni mwa mabingwa!!

tetesi, Tetesi za Soka Barani Ulaya., Meridianbet

CHEZA HAPA

ONI MOJA

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa