Chelsea wamefanikiwa kuingia fainali ya Ligi ya Mabingwa baada ya kuibwaga Real Madrid kwa 2-0 siku ya Jumatano na kukamilisha jumla ya magoli 3-1 katika hatua ya nusu fainali.

Chelsea Watinga Fainali ya Champions League

Timu ya Thomas Tuchel sasa itakutana na Manchester City huko Instanbul baada ya kupata ushindi wa kustahili huko Stamford mabao ya Timo Werner na Mason Mount.

Hii inakuwa fainali ya pili mfululizo kwa Thomas Tuchel katika michuano hiyo baada ya kuifikisha PSG msimu uliyopita na kupoteza kwa 1-0 dhidi ya Bayern Munich.

Real Madrid walifurahia umiliki wa mpira kwa 73% dakika 25 za kwanza na Edouard alikuwa imara langoni kwa kuokoa shuti kali lililopigwa na Kareem Benzema.

Ngolo Kante alimtengenezea Kai Harvetz pasi safi ambayo alichop mpira ulioenda kugonga besela na kumliziwa kwa kichwa na Werner na kufanya ubao usome 1-0 kipindi cha kwanza chas mchezo.

Kante pia alipoteza nafasi ya kufunga kabla ya Mount kufunga bao la pili pasi safi kutoka kwa Christian Pulisic hakika vijana wa Tuchel waliisumbua ngome ya Los Blancos.

Nini kinafuata?

Chelsea watakabiliana na timu ya Pep Guardiola Man City mchezo wa Premier League siku ya Jumamosi, mchezo ambao kwa namna fulani unaweza kutoa taswira ya nani anaweza kuwa bingwa Champions League pindi watakapo kutana tena kwenye fainali hiyo.


TENGENEZA FAIDA KUPITIA MCHEZO WA TITAN DICE UKIWA NA MERIDIANBET KASINO

Unapokuwa kwenye Kasino ya Mtandaoni ya Meridianbet, huna sababu ya kucheza kwa mashaka. Titan Dice, ni mchezo unaweza kukupatia mamilioni kwa mzunguko mmoja!

Chelsea, Chelsea Watinga Fainali ya Champions League, Meridianbet

SOMA ZAIDI

12 MAONI

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa