Kwa wiki nyingine klabu ya Chelsea imeendelea kutamba kunako Premier League na kuzidi kujikita kileleni mwa ligi hiyo baada ya kuinyuka Norwich 7-0 katika dimba la Stamford Bridge, wakati Mason Mount akiondoka na mpira kwa kufunga hat-trick.

Chelsea Yaishushia Kipigo cha 7-0 Norwich

Ulikuwa ni mchezo uliyo wakutanisha viongozi wa ligi na washika mkia wa ligi ambapo Mount alifungua ukurasa wa mabao dakika ya 8 ya mchezo wakati Callum Hudson-Odoi akiweka bao la pili dakika ya 18 na Reece James aliweka chuma ya tatu kabla ya kwenda mapumziko.

Ben Chilwell aliendelea na utaratibu wake wa kufunga kila mechi kwa kuweka kimiani bao namba 5 kabla ya Max Aaron kujifunga dakika ya 62, zikiwa zimesalia dakika tano mpira kumalizika Chelsea walipata penati ambayo ilifungwa na Mount na kukamilisha ushindi wa goli 7 na hat-trick dakika za nyongeza.

The Blues sasa wamejikita kileleni wakiwa wamekusanya jumla ya alama 22 katika michezo 9 wakifuatiwa na Liverpool pointi 18 ambao watakabiliana na Man United siku ya Jumapili jioni.


KUSANYA MKWANJA NA BIG BAD WOLF

Mchezo wa Big Bad Wolf ni moja ya michezo pendwa katika kasino zetu za meridianbet. Ukiachana na tabasamu utakalolipata wakati wa kucheza pia unajiwekea nafasi ya kuwa mshindi wa mkwanja mrefu unaotoka kila baada ya mzunguko kukamilika.

tetesi, Tetesi za Soka Barani Ulaya., Meridianbet

CHEZA SASA

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa