Chelsea wameingia katika kinyang’anyiro cha kumtaka Georginio Wijnaldum ambaye yupo kwenye mipango ya Barcelona katika dirisha la kiangazi.
Chelsea Yaunga Tela Kuitaka Saini ya Wijnaldum
Kiungo wa Liverpool Geoginio Wijnaldum

Kiungo wa Liverpool amehakikishiwa kuungana na mtaifa mwenzake Ronald Koeman huko Camp Nou baada ya mkataba wake kufika tamati.

Jurgen Klopp alikuwa akiamini atambakisha muholanzi lakini mazungumzo yameshindikana katika ya mchezaji na Klabu.

Na ilikuwa ikiripotiwa Uhamisho wa Wijnaldum wa kwenda Barcelona ulikuwa umefanyika kwa asilimia 95 baada ya sababu za kiuchumi ilimaanisha walimkosa msimu uliyopita.

Lakini Marca imeandika jinsi klabu hiyo ya Premier League wamejiunga katika orodha ya vilabu vinavyo winda saini ya mchezaji huyo Juventus na Paris Saint-Germain vikijumuishwa.

Usajili wa kiangazi utampa fursa kocha wa sasa wa Chelsea Thomas Tuchel kufanya usajili wake wa kwanza baada ya kuchaguliwa kukuchua mikoba ya aliyekuwa kocha wa The Blues Frank Lampard baada ya kutimuliwa mwezi Januari mwishoni.

Wijnaldum mwenye umri wa miaka 30 anajiandaa kuondoka Liverpool baada ya kuitumikia klabu hiyo kwa kipindi cha miaka mitano.

Alifanikiwa kunyanyua taji la Premier League msimu uliyopita baada ya kufanikiwa kushinda taji la Champions League na Club World Cup.


UNAWEZAJE KUKOSA KASINO YA BREAK AWAY LUCKY WILDS INAYOKUPA NAFASI YA USHINDI MURUA.

Break Away Lucky Wilds ni moja ya Sloti pendwa katika kasino za #meridianbet inayokupa mara 11,000X ya dau lako, unayo nafasi ya kuwa milionea unasubiri nini?

CHEZA HAPA

5 MAONI

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa