Wapenzi wa soka wanajua ni raha sana kushuhudia timu ikishinda kutokea nyuma, yaani inapigwa goli kadhaa na kurudisha zote kisha kupata nyongeza ya magoli ya ushindi!

Hii ndiyo sisi tunaiita comebacks!

Ligi ya Mabingwa, Champions League imekuwa na mambo mengi sana ya kukumbukwa kwa hakika kabisa. Kuanzia kwenye mabao maridadi mno hadi kwenye uchezaji unaoburudisha sana machoni, ligi kubwa hiyo ya huko Ulaya imekuwa nzuri mno. Hata hivyo, comebacks za Champions League zimekuwa za aina yake.

Hapa utaona baadhi ya comebacks ambazo zilitikisa ulimwengu wa kandanda:

Tunaendelea…

2004: Deportivo La Coruna 4 v 0 AC Milan

Mwaka 2004, klabu ya huko Hispania, Deportivo la Coruna ilikuwa ni moja ya klabu kubwa sana. Walikuwa wanalinda taji la moja ya misimu iliyopita. Walikuwa wanatishia sana maisha ya klabu za Barcelona na Real Madrid pamoja na utawala wao katika ligi. Pia, walikuwa wanatishia sana katika mbio za kutwaa taji na wakavunja utawala wao mwaka 2000 wakati waliposhinda taji la ligi ya La Liga, Hispania.

Mabingwa waliokuwa wanachipukia wakati huo, Milan waliwatandika Deportivo 4-1 katika mechi zao za kwanza wakiwa pale dimbani San Siro. Kwa matokeo hayo, hao Deportivo walidhani wamemaliza kazi, au siyo? Umekosea!

Upande wa Javier Irureta ulishangazwa na kuaibishwa sana. Kikosi cha Ancelotti kilitandaza soka tamu sana na lenye kupendeza mno. Mchezaji Walter Pandiani alifungua karamu ya mabao kwa kufunga dakika za mwanzo kabisa. Naye Juan Carlos Valeron alifunga bao la pili dakika ya 34 wakati naye Albert Luque alipita na bao la 3 na matokeo kuwa ni 3-0 kabla ya kwenda half time. Milan hawakuweza kurudisha ari yao na kuepuka kichapo kwani Fran alimaliza kazi mapema kabisa kwa kuweka kimiani goli la nne katika dakika ya 76 ya mchezo.

Ingawa kwa sasa wanapambana na hali yao huko kwenye ligi daraja la pili la Hispania ila waliacha alama ya pekee sana na ya kukumbukwa katika michano ya soka ya Champions League.

2019: Liverpool 4 Barcelona 0

Wakongwe hawa wawili wa barani Ulaya wamezalisha mambo mengi sana ya kukumbukwa kwenye michuano hii. Lakini mwaka jana comeback ya klabu ya soka ya Liverpool ilibamba mno, mno! Wakiwa na matokeo ya 3-0 katika mechi yao ya kwanza, klabu ya soka ya Liverpool walikutana na kigingi kikubwa kutoka kwa kikosi cha Lionel Messi aliyekuwa na wenzake wa Barcelona.

Hao The Reds waliingia katika mechi bila ya huduma ya wachezaji wao kama akina Mohamed Salah pamoja na Roberto Firmino. Ilikuwa mshike mshike sana katika comeback hii ya hatua ya nusu fainali za mashindano hayo.

Lionel Messi, aliyefunga mabao mawili katika mechi ya marudiano hakuwa akionekana kabisa katika mechi na ikawa nafasi ya Liverpool kuwachabanga hao Barcelona 4-0 ambapo wakapaa mpaka kwenye hatua ya kutwaa taji lao la sita la ligi kubwa huko barani Ulaya.

51 MAONI

  1. Inavutia sana mana timu nyingine zikiwa zinajua kuwa washashinda basi wanajiachia sana katika mchezo ndipo wanapo wapa upenyo wapizani wao kushinda

  2. Comeback hatari ni Liverpool vs Milan 2005 pale turkey ilikiwa fanail Bora Liverpool alishinda kwa penalty# meridianbettz.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa