Inadaiwa kuwa klabu ya Inter Milan wanaweza kumsajili nyota wa Real Madrid Gareth Bale kwenye dirisha hili la msimu wa joto.

Kwa mujibu wa kituo kimoja cha televisheni nchini Italia, Conte amemuomba mkurugenzi mkuu wa klabu Beppe Marotta na mkurugenzi wa michezo Piero Ausilio kumleta bale klabuni hapo.

Nyota huyu mwenye miaka 29 amekuwa kwenye sintofahamu ya hatma yake klabuni Real Madrid baada ya meneja Zinedine Zidane kuweka wazi kuwa hamuhitaji mchezaji huyo kwa msimu ujao. Bale alishawahi kuwapiga Inter mabao 3 kabla hajajiunga na Real Madrid mwaka 2010.

Kama nyota huyu ataenda Inter huenda ikawa ni neema kuliko kusalia Real Madrid, ambako Zidane anasisitiza kuwa hana kazi msimu ujao. Wakala wa mchezaji huyu alidai kuwa staa huyu atabakia Real licha ya maneno ya bosi.

Inter Milan wanatarajia kusajili wachezaji wengi bora kiangazi hiki ikiwa ni maandalizi ya kupambana vyema kwenye Ligi ya Mabingwa msimu ujao.

Bale amefunga jumla ya magoli 102 na pasi 64 kwa kipindi chote cha miaka 6 alichokuwepo klabuni hapo licha ya kushindwa kuteka vyema mioyo ya mashabiki wa Real Madrid.

ONI MOJA

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa