Nchi ya Colombia inakosa bahati ya kuingia kwenye historia ya mashindano ya Copa America. Maandamano yanayoendelea nchini humo, yamekuwa kikwazo kikubwa.

Kwa mara ya kwanza kwenye historia ya miaka 105 tangu kuanzishwa kwa mashindano ya Copa America, nchi 2 zingehusika kusimamia mashindano hayo. Colombia na Argentina zilipata fursa ya kuongoza mashindano hayo yanayohusisha timu 10.

Kumekuwa na maandamano makubwa nchini Colombia ambapo waandamanaji wanaishutumu vikali serikali ya nchi hiyo. Kutokana na maandamano haya, baadhi ya michezo ya Copa Libertadores imethirika na hivyo shirikisho la soka barani Amerika Kusini, limeamua kuiondoa Colombia kwenye orodha ya nchi itayosimamia mashindano hayo.

“Tunatambua uwepo wa Copa America 2021 na kwa siku chache zijazo tutatangaza mabadiliko ya sehemu ambazo michezo iliyokuwa imepangwa kuchezwa Colombia itapofanyika” Shirikisho la soka America Kusini limeripoti.


UNAWEZA KUWA MILIONEA WAKATI WOWOTE!

Zungusha na ushinde mkwanja wako papo hapo baada ya mzunguko kukamilika. Ni kugusa tu 🤑.

River Plate, River Plate, Enzo Perez Aonesha Uwezo Golini., MeridianbetBASHIRI SASA

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa