Mshambuliaji wa Bayern Munich Philippe Coutinho amesisitiza anauzingatia mchezo wa fainali kwanza hali ya kuwa yupo kwenye mazungumzo juu ya uhamisho wake.

Coutinho atacheza mchezo wake wa mwisho katika timu ya Bayern Munich dhidi ya Paris Saint-Germain katika fainali ya Champons League siku ya Jumapili kabla hajarudi katika klabu yake ya Barcelona.

Lakini mchezaji huyo wa kimataifa wa Brazil anatarajia kuondoka Barcelona kwa uhamisho wa moja kwa moja amekuwa akihusishwa na kujiunga na Arsenal.

Lakini Coutinho, aliyetua Barcelona akitokea Liverpool mwezi Januari 2018, amesema kwa wakati huu mawazo yake ameyaelekeza kwenye mchezo wa Jumapili dhidi ya PSG.

COUTINHO, Coutinho Azingatia Fainali ya UEFA Kwanza., Meridianbet

“Akili yangu inafikiria na nimeielekeza katika mashindano,” aliiambia Esporte Interativo mchezaji huyo.

“Ni fursa ya kipekee kwetu sisi, nina furaha kuwa sehemu ya kikosi kitakacho cheza fainali ya Champions League.

“Kuhusu hatima yangu sijafikiria kwa sasa kwa sababu ninacho kiwaza ni fainali ya Jumapili tu.”

Coutinho amefunga goli 11 na kutoa pasi za mabao 9 katika michezo 37 kwenye mashindano yote akiwa na Bayern Munich mwaka 2019-20.


Drops and Wins!

Umeijua hii? Ni promosheni kabambe ya ushindi kwenye Casino ya mtandaoni ya Meridianbet! Unaweza kushinda hadi Euro 2,000,000 leo.

Soma zaidi ucheze

40 MAONI

  1. Maisha hayajawahi kuwa sawa kwa Coutinho tangu kuwa nyota anayetegemewa akiwa Liverpool hadi kucheza kwa mkopo kwasababu ya kutokuwa na kiwango#meridianbettz

  2. Ni kweli lazima afikirie kwanza mchezo wa fainali kwani wakichukua kombe utampa heshima kubwa,vile vile naona ahame Barcelona kwani si timu sahihi kwake akija Arsenal itakua vizri ila tatizo Arsenal sidhani kama watamwaga mpunga mnene kwake vinginevyo wamuuze Ozil ambae nae inakua vigumu kwani Arsenal inataka dau nono

  3. Kweli kabisa kuzingatia mchezo unao kuja nilazima mana unafaida ndani yake kumletea heshima sana.yuko vizuri namkubali

  4. Maisha hayajawahi kuwa sawa kwa Coutinho tangu kuwa nyota anayetegemewa akiwa Liverpool hadi kucheza kwa mkopo kwasababu ya kutokuwa na kiwango

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa