Cristiano Ronaldo ataendelea kuwa nahodha wa Ureno licha ya kuonyesha hisia kali katika mchezo uliopita na Serbia”, anasema Kocha wa timu hiyo Fernando Santos.

Mshambuliaji huyo alitoka uwanjani sekunde chache kabla ya filimbi ya mwisho na kupewa kadi ya njano baada ya goli kukataliwa siku ya Jumamosi na matokeo yalikuwa draw ya 2 – 2.

Cristiano Ronaldo Kuendelea Kuwa Nahodha wa Ureno.
Cristiano Ronaldo Kuendelea Kuwa Nahodha wa Ureno.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 36 aliachwa akikasirika wakati juhudi yake iliondolewa na beki wa Serbia Stefan Mitrovic kuutoa mpira ndani ya mstari wa goli.

Bila ya kuwepo kwa Mwamuzi msaidizi wa Video (VAR) ama teknologia yeyote ya kuonyesha goli. Mwamuzi wa Kihoranzi Danny Makkelie alipeperusha kibendela kwa ishara ya mchezo kuendelea, Ronaldo alikivua kitambaa cha unahodha na kukitupa huku akitoka uwanjani kuelekea kwenye chumba cha wachezaji.

“Ndiyo, ataendelea kukivaa kitambaa cha Unahodha milele,” alisema Santos. “Cristiano (Ronaldo) ni mfano wa kitaifa.

“Ikiwa angemkosea meneja, wachezaji wenzake au shirikisho kwa tabia aliyoionyesha, basi tungelazimika kulizungumzia hili swala, lakini hakuna kitu kama hicho kilichotokea.Cristiano Ronaldo.

“Ulikuwa wakati wa kuchanganyikiwa sana. Na tunazungumza juu ya mchezaji ambaye hashindwi na chochote wakati anapotaka kushinda.

“Hakuna mtu atakayesema kwa sasa kuwa alichokifanya Ronaldo ni kizuri, lakini hakukuwa na maana ya kujadili kama Cristiano aendelee kuwa nahodha wa timu hii. Na hicho ndio kitu ambacho nataka kukiweka wazi.”

Baadaye Ronaldo aliingia kwenye mtandao wa kijamii wa Instagram kutoa wasiwasi wake, akichapisha: “Daima ninatoa na nitatoa kila kitu kwa nchi yangu, hiyo haitabadilika kamwe.

“Lakini kuna nyakati ngumu kushughulika nazo, haswa wakati tunahisi kuwa taifa zima linaumizwa.

“Tutaweka vichwa vyetu juu na kukabiliana na changamoto inayofuata sasa.”

UEFA baadaye ilisema goli la Ronaldo lingesimama ikiwa bodi zote za uongozi za Serbia na Ureno zilikubaliana kabla ya mchezo kutumia teknolojia ya safu ya mabao (VAR).


UNAWEZAJE KUKOSA KASINO YA BREAK AWAY LUCKY WILDS INAYOKUPA NAFASI YA USHINDI MURUA.

Break Away Lucky Wilds ni moja ya Sloti pendwa katika kasino za #meridianbet inayokupa mara 11,000X ya dau lako, unayo nafasi ya kuwa milionea unasubiri nini?

cristiano ronaldo, Cristiano Ronaldo Kuendelea Kuwa Nahodha wa Ureno, Meridianbet

CHEZA HAPA

7 MAONI

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa