Trent Alexander-Arnold alilazimika kutolewa njre ya dimba mwishoni mwa mchezo wa England wa 1-0 dhidi ya Austria huko Middlesbrough Jumatano jioni, na kuweka mashaka juu ya ushiriki wake kwenye Mashindano ya Euro 2020.

Alexander-Arnold Shakani Kuikosa Euro 2020

Bosi wa England Gareth Southgate alielezea baadaye kwamba anaamini kuumia ni kwa paja la mchezaji, lakini kwamba tatizo kamili litajulikana kwa masaa mengine 24-48.

Southgate alichagua kikosoi cha XI ya majaribio, na Tyrone Mings na Conor Coady wote wakianzia beki wa kati, pamoja na beki wa kulia wa Liverpool na Kieran Trippier wa Atletico Madrid.

Jude Bellingham, Jack Grealish na Declan Rice pia walianza, vile vile Harry Kane na Jesse Lingard, ingawa wa mwisho hawakujumuishwa kwenye kikosi cha mashindano hayo. Bukayo Saka wa Arsenal pia alishiriki kwenye XI na akafunga bao pekee la mchezo.

Lakini stori ya usiku bila shaka ilikuwa jeraha la Alexander-Arnold, ambalo limekuja siku moja tu baada ya kikosi kutangazwa.

Mchezo wa kwanza wa England kwenye Euro 2020 ni dhidi ya Croatia utakuwa mwezi Juni 13.


MAANA KAMILI YA USHINDI KATIKA KASINO ZA MERIDIANBETI NI PAMOJA NA MCHEZO WA PANDA PANDA.

Hii ndiyo burudani yenye ushindi! Ingia kwenye kasino ya Meridianbet kufukuzia ushindi huu. Cheza sasa Panda Panda na uwe moja ya washindi na Mabingwa.

Gomes, Gomes : Sitafanya Usajili wa Kutisha., Meridianbet

CHEZA HAPA

ONI MOJA

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa