Arsenal wanaripotiwa bado hawajafanya mawasiliano na Norwich City kuhusu mpango wa uhamisho wa kiungo Emiliano Buendia.

Washika bunduki wanasaka wachezaji wabunifu na wanaendelea kuhusishwa na wachezaji kama Houssem Aouar na Dominik Szoboszlai.

Arsenal pia inasemekana inavutiwa na Buendia, ambaye kwa nafasi yake alifanya vyema katika msimu mbaya wa Norwich wa Ligi Kuu ya Uingereza 2019-20, na mchezaji huyo wa miaka 23 tayari anajivunia mabao mawili na asisti tano kwenye kampeni ya sasa ya Championship.

emiliano buendia

Hata hivyo, kulingana na Football London, Arsenal hawajafanya mawasiliano rasmi juu ya Muargentina huyo, ingawa ni mchezaji ambaye Mikel Arteta anamkubali.

Ripoti hiyo inadai kwamba Buendia anazingatia tu kuwasaidia Norwich kurejea haraka kwenye Ligi ya Premia, lakini ikiwa Norwich haitapokea ofa ya kiungo huyo mnamo Januari, Buendia hafikirii kufanya uhamisho.

Buendia yuko chini ya mkataba na klabu ya Norwich hadi mwisho wa msimu wa 2023-24.


 

FURAHIA MUZIKI MTANDAONI HUKU UKITENGEZA MKWANJA!!

Mchezo wa Astro Legend unakupatia burudani ya muziki kupitia kasino ya mtandaoni ya Meridianbet. Utaburudika huku ukiendelea kutengeza mkwanja mrefu, jiunge sasa na uwe miongoni mwa mabingwa!!

Arsenal, Arsenal Wamefanya Lolote Juu ya Emiliano Buendia?, Meridianbet

INGIA MCHEZONI

18 MAONI

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa