Arsenal Wang'aa Debi ya London Dhidi ya Spurs

Arsenal waliinyuka Tottenham ambao ni mahasimu wao wa jijini upande wa kaskazini mwa London bao 3-1 katika mchezo wa wiki ya sita katika Premier League siku ya Jumapili jioni.

Arsenal ambao wakuwa na fomu nzuri siku za hivi karibuni walipata magoli matatu ndani ya kipindi cha kwanza Emile Smith-Rowe akifunga bao la ufunguzi katika dakika ya 12 baada ya kupokea pasi kutoka kwa Bukayo Saka, kabla ya Pierre-Emerick Aubameyang kuweka bao la pili dakika ya 28 na goli la tatu likiwekwa kimiani na Bukayo Saka. Bao la kufutia machozi kwa Spurs lilifugwa na Heung-Min Son dakika ya 79 ya mchezo.

Katika mchezo huo Spurs waliweka historia ya kuruhusu kufungwa magoli matatu au zaidi mfulululizo katika EPL kwa mara ya kwanza tangu mwaka 2003.

Arsenal sasa wamesogea mpaka nafasi ya kumi kwenye msimamo wa Premier Laegue wakiwa wakusanya jumla ya alama 9 kutoka katika michezo sita ya ufunguzi.


FUNGA BAHATI YAKO NA MERIDIANBET.

Ni wakati wa ushindi mkubwa ukiwa na kasino bomba ya Lock a Luck, meridianbet wanakupa sababu ya ushindi, funga bahati yako ya ushindi ukiwa na mabingwa.

tetesi, Tetesi za Soka Barani Ulaya., Meridianbet

CHEZA HAPA

 

 

Acha ujumbe