Tetesi zinadai Arsenal wanataka kusajili wachezaji wawili kama mbadala wa Alexander Lacazette wachezaji hao ni Ollie Watkins na Dominic Calvert-Lewin ingawa wachezaji wote bado hawafikii ubora wa Mfaransa huyo.

Lacazette atakuwa nje ya mkataba mwishoni mwa msimu huu na anaweza kuuzwa katika dirisha la Januari ili kuepuka kumuacha aondoke bure.
Lakini mkuu wa Arsenal anania ya kumsajili mshambuliaji wa Everton Calvert-Lewin ambaye ana umri wa miaka 24 vilevile foawdi wa Aston Villa Watkins mwenye umri wa miaka 25 kwaajili ya kuziba pengo.

Clavert-Lewin na Watkins wamecheza michezo mingi zaidi ya Lacazette katika Premier League lakini licha ya kuzidiwa mechi na wachezaji hao Lacazette amefunga mabao mengi zaidi yao. Lacazette amefunga mabao 50 wakati Calvert-Lewin amefunga mara 42 huku Watkins akiweka kambani mabao 15.
SPACE SPIN NA MERIDIANBET.
Ni Mabingwa pekee Meridianbet wanakupa nafasi ya kushinda zaidi na mchezo wa Space Spin katika kasino bomba za meridianbet. Ni wakati wa kufurahia na kutengeza mkwanja bila kuwaza.


