Timu ya Arsenal iliibuka na ushindi mnono wa 3-1 dhidi ya Manchester United katika dimba la Emirates na kurejesha matumaini ya kucheza Ligi ya Mabingwa msimu ujao.

Magoli ya Arsenal yalifungwa na Nuno Tavares ambaye alimalizia mpira uliyotemwa na De Gea baada ya kujaribu kuokoa mpira wa hatari wakati bao la pili liliwekwa kimiani na Saka kwa mkwaju wa penati na bao la kufutia machozi kwa United lilifungwa na Ronaldo kabla ya kwenda mapumziko.

Dakika ya 70 Xhaka aliangamiza ngome ya Rangnick kwa shuti kali nje ya eneo la penati na kufanya 3-1 kwa Arsenal wakati Bruno Fernandes alikosa penati baada ya mchezaji wa The Gunners kuunawa mpira.

Kupoteza kwa United kinakuwa kipigo cha pili mfululizo baada ya kupoteza kwa Liverpool 4-0 mwanzoni mwa wiki na sasa Mashetani wekundu wamesalia katika nafasi ya sita wakiwa na jumla ya alama 54 katika michezo 34.

Goli la Christiano Ronaldo lilifanya afikishe idadi ya mabao 100 katika Premier League.


TENGENEZA FAIDA NA ZEUS ANCIENT FORTUNES

Una Kila sababu ya kufurahia wiki yako na kutengeneza mwaka huu uwe wa faida zaidi katika kasino zetu za mtandaoni za meridianbettz. Mchezo wa Zeus Ancient Fortunes unakuongoza kutekeleza hilo.

tetesi, Tetesi za Soka Barani Ulaya., Meridianbet

CHEZA HAPA

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa