Pierre-Emerick Aubameyang alikosa moja ya nafasi nyepesi ambayo ahajawahi kuipata katika mchezo waliyo kwenda sare ya 1-1 na Benfica katika Europa League siku ya Alhamisi akiunganisha mpira kwenye wavu kipindi cha kwanza nje ya box ya yadi sita.
Aubameyang Aomba Radhi kwa Kupata Sare na Benfica.
Bukayo Saka akishangilia baada ya kufunga dhidi ya Benfica kwenye michuano ya Ligi ya Uropa.

Fowadi huyo wa Arsenal, ambaye pia alipigiwa firimbi ya kuotea mara nne, anajua uchezaji wake wa chini ya kiwango uliweza kuigharimu timu. Gunners labda wanahitaji kushinda mashindano hayo ya Europa League ili kufuzu kushiriki Ligi ya Mabingwa mwakani kutokana na msimamo wao katika jedwali la ligi ya nyumbani,

Aubameyang aliomba msamaha kwa kupoteza kwake nafasi kadhaa kwenye mitandao ya kijamii kufuatia mechi hiyo.

“Tulistahili ushindi na ningepaswa kufunga mabao kadhaa leo lakini bado tuna mchezo wa kurudiana tunaendelea,” Aubameyang aliandika kwenye Twitter.

Mikel Arteta alinena juu ya Aubameyang kukosa nafasi kwenye mchezo huo: “Sawa, haya mambo hufanyika,” Arteta alisema. “Alikuwa mwisho wa nafasi kubwa zaidi ambazo tulikuwa nazo usiku wa leo.

“Hakuwa na bahati ya kufunga leo angefunga bao mbili au tatu usiku wa leo kwa sababu katika hali ya kawaida ndivyo ilitakiwakuwa.”


WEWE NI SHUJAA? MASHUJAA WANASHINDA HAPA!

Treasure Heroes inakupa nafasi ya kupambania ushindi wako mkubwa kwenye kasino ya mtandaoni ya Meridianbet! Usisubiri hii, jiunge sasa kufurahia ushindi!

Kasino ya Mtandaoni

INGIA MCHEZONI

12 MAONI

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa