Baba wa mshambuliaji wa PSG Lionel Messi amesema anatumaini kwamba mchezaji huyo atarejea kwenye klabu yake ya zamani Barcelona.

Kulikuwa na uvumi kwamba nyota huyo wa kimataifa wa Argentina atarejea Camp Nou na baba yake ni kama ameongeza moto kwenye tetesi hizo.

Messi aliondoka kama mchezaji huru na kujiunga na Paris Saint-Germain msimu uliyopita baada ya mkataba wake kuisha na Barca hawakumpa mkataba mpya sababu ya matatizo ya kifedha.

Lakini mara baada ya Xavi kuteuliwa kuwa kocha mkuu wa Barcelona alisema milango ipo wazi kwa nyota huyo kama akihitaji kurejea katika klabu yake iliyomkuza.

Babake Messi, Jorge, aliulizwa na kituo cha Twitch cha Jijantes FC kuhusu uwezekano wa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 34 kuvaa jezi ya Blaugrana tena.

Akajibu: “Natumai itatokea, siku moja.”


TENGENEZA FAIDA NA ZEUS ANCIENT FORTUNES

Una Kila sababu ya kufurahia wiki yako na kutengeneza mwaka huu uwe wa faida zaidi katika kasino zetu za mtandaoni za meridianbettz. Mchezo wa Zeus Ancient Fortunes unakuongoza kutekeleza hilo.

tetesi, Tetesi za Soka Barani Ulaya., Meridianbet

CHEZA HAPA

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa