Barcelona Kutoana Jasho na Madrid kwa Endrick

Miamba wa LaLiga Real Madrid na Barcelona wanavutiwa kumsajili kinda wa miaka 15 Endrick Felipe Moreira na tayari mchezaji huyo wa klabu ya Palmeiras yupo kwenye rada za matajiri hao wa Hispania.

Barcelona Kutoana Jasho na Madrid kwa Endrick

Hakuna klabu yoyote itakayoweza kumsajili kwa sasa, kwani FIFA hairuhusu vilabu kupata huduma za wachezaji wa nje walio na umri wa chini ya miaka 18. Hata hivyo, Blaugrana na Los Blancos wana nia ya kuanzisha vita ya kuinasa saini ya kinda huyo siku zijazo.

Siku chache zilizopita, Endrick alifunga bao kali dhidi ya Oeste na kuisaidia Palmeiras kufuzu nusu fainali ya Copinha – mchuano unaoleta pamoja vijana wenye vipaji bora zaidi nchini Brazil na ambao wachezaji kama Neymar, Vinicius na Casemiro walionekana siku za nyuma.

Endrick hakufanikiwa kutinga wavuni kwenye nusu fainali dhidi ya Sao Paulo, lakini atapata nafasi nyingine ya kufanya hivyo kwenye fainali na Santos Jumanne.

Akiwa na urefu wa mita 1.73 akiwa na umri wa miaka 15, mshambuliaji huyo anayetumia mguu wa kushoto ana wastani wa kufunga bao moja kwa mechi katika michezo yake zaidi ya 150 aliyoichezea timu ya vijana ya Palmeiras, huku Nike wakiwa tayari wamefikia makubaliano ya kumdhamini mchezaji huyo.


JIACHIE NA ALMIGHTY AZTEC

Ni muda wako kujiachia na mchezo maridhawa wa Almighty Aztec katika kasino bomba za meridianbettz. Nafasi ya kutengeneza mkwanja iko mikononi mwako kazi ni kwako.

tetesi, Tetesi za Soka Barani Ulaya., Meridianbet

CHEZA HAPA

Acha ujumbe