Mabosi wa Klabu ya Barcelona wanamfuatilia kwa ukaribu nyota wa Borussia Dortmund, Erling Haaland ili kupata saini yake.

Barcelona wanahitaji kupata saini ya Haaland mwenye miaka 20 ili kuongeza nguvu ndani ya kikosi hicho kwa ajili ya kumlinda nyota wao Lionel Messi ili abaki msimu ujao kwa kuwa imekuwa inaripotiwa kwamba anahitaji kuondoka.

BarcelonaKwa kufanya hivyo Barcelona itakuwa imeingia kwenye vita na wapinzani wao ndani ya La Liga ambao ni Real Madrid na timu nyingine ambazo zinashiriki Ligi Kuu England ambazo ni pamoja na Manchester United, Manchester City na Chelsea  ambazo zinazoripotiwa kuhitaji saini yake.

Mshambuliaji huyo amekuwa na rekodi bora ambapo amefunga jumla ya mabao 55 katika jumla ya mechi 57 ambazo amecheza jambo ambalo linafanya thamani yake izidi kuwa kubwa ambapo imeripotiwa kwamba mabosi wake wa sasa wa Dortmund wamesema kuwa kuipata saini ya nyota huyo sio chini ya euro milioni 154.


Unaweza kuwa milionea wakati wowote!

Zungusha na ushinde mkwanja wako papo hapo baada ya mzunguko kukamilika. Ni kugusa tu 🤑.

barcelona, Barcelona Yampigia Mahesabu Haaland, MeridianbetBASHIRI SASA

2 MAONI

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa