Mshambuliaji wa Real Madrid Karim Benzema amekaribia kuipita rekodi ya Robert Lewandowski ya mabao katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya baada ya kufunga mara mbili katika mchezo wa kupoteza kwa 4-3 dhidi ya manchester City siku ya Jumanne.

Real Madrid ilikuwa ugenini kwa Manchester City katika mchezo wa nusu fainali ya kwanza ya Ligi ya Mabingwa mchezo ambao Los Blancos ilikubali kipigo cha 4-3 benzema akicheka na nyavu mara mbili na kufikisha jumla ya mabao 85 bao moja nyuma ya Lewandowski ambaye anashika tatu kwa wafungaji bora wa muda wote.

Benzema amecheza jumla ya mechi 140 katika Champions League na kwa sasa yeye ndiye anaongoza kwa mabao msimu huu akiwa na jumla ya mabao 14 akifuataiwa na Lewandowski ambaye anamagoli 13 na tayari wametolewa kwenye michuano.

Orodha ya 5 bora ya wafungaji wa muda wote kwenye Ligi ya Mabingwa.

  1. Christiano Ronaldo  –  140

2. Lionel Messi – 125

3. Robert Leandowski –  86

4. Karim Benzema  –  85

5. Raul Gonzalez  –  71

BASHIRI MECHI ZA LEO ZA HAPA

 

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa