Bravo Aondoka Manchester City.

klabu ya Premier League, Manchester City imethibitisha kuondoka kwa Claudio Bravo baada ya kumaliza mkataba na klabu hiyo.

Mlinda mlango huyo mwenye umri wa miaka 37 alijiunga na Manchester City akitokea Barcelona mwaka 2016 baada ya kukaa miaka miwili na Blaugrana.

Bravo alitua City muda mfupi baada ya Pep Guardiola kuajiliwa na mabingwa hao wa Uingereza na kupandikiza Falsafa za kikatalani za kupiga mpira mwingi.

Guardiola alimpa nafasi kubwa Bravo kutokana na kupendelea ujuzi wa kipa huyo kwa kuwa na uwezo wa kucheza pasi hivyo basi kuwa chaguo namba moja la Guardiola na alikuwa akisaidiana na Joe Hart ambaye alicheza michezo 30 katika mashindano yote.

Kiwango cha Bravo kilikuwa thabiti na amemaliza muda wake katika klabu ya City akisaidiana na Ederson aliyesajiliwa kutokea timu ya Benifica mwaka 2017.

Bravo ameondoka City akiwa amefanikiwa kushinda makombe mawili ya Premier League na EFL Cup mbili.

Wakati ikiwa haijulikani wapi ataelekea, Bravo amekuwa akihusishwa mara kwa mara na kujiunga na Celtic na Real Betis, ambayo itakuwa inafundishwa na mwalimu wa zamani wa Manchester City kocha Manuel Pellegrini msimu ujao.


Drops and Wins!

Umeijua hii? Ni promosheni kabambe ya ushindi kwenye Casino ya mtandaoni ya Meridianbet! Unaweza kushinda hadi Euro 2,000,000 leo.

Soma zaidi ucheze

40 Komentara

    Nivizuri kubadilisha upepo kambi kokote

    Jibu

    Bravo sasa anaweza akachukuliwa club yoyote maana yupo huru

    Jibu

    Bravo Ni kipa bora wamemkosa man city

    Jibu

    Kila la kheri Bravo

    Jibu

    kila la kheri uendapo

    Jibu

    Safari njema

    Jibu

    Popote kambi

    Jibu

    Claudio Bravo aliitumikia vyema man city namtakia kila la kheri huko aendako

    Jibu

    Mambo mengi sana hameifanya clabu ya man city hadi kufikia nusu fainali kila la goli kipa makini sana bravo

    Jibu

    Yuko vzuri kila la kheri aendapo

    Jibu

    Kila la heri bravo ni muda sasa wakufanya juhudi ili uwe kipa bora mana bado mambo magumu kwako hata kama umejitahidi kuingia nusu fainali

    Jibu

    Bravo ameonekana kushuka sana kiwango

    Jibu

    Nenda kapambane sehemu nyingine.

    Jibu

    Duh sikujua kwamba bravo yuko man city anahaki ya kusepa.

    Jibu

    Safari njema kwake

    Jibu

    Safi kutafuta chaka lingine

    Jibu

    Duh kila la kheri BRAVO unaondoka CITY bado inakudai TAJi la UEFA Ila kila la kheri BRAVO bye bye๐Ÿงค๐Ÿงค๐Ÿงค

    Jibu

    Kapambane

    Jibu

    Bravo japo umri umeenda ila yuko vzur sana

    Jibu

    Kila la heri

    Jibu

    Amekaa Sana benchi Ni vizuri atafute sehemu nyingine ambayo atakua anaweza kucheza Kama namba moja

    Jibu

    Kila lakheri

    Jibu

    Kwaher

    Jibu

    Safi

    Jibu

    I we kheri huko aendako.

    Jibu

    Kila la kheri bravo

    Jibu

    Nenda kaka kila la kheri maisha popote

    Jibu

    kila la kheri bravo uko uendako

    Jibu

    Kila la kheri bravo

    Jibu

    Nenda tu kaka maisha popote
    @meridianbet

    Jibu

    Kikubwa riziki

    Jibu

    Bravo ameonekana kushuka sana kiwango

    Jibu

    Safi maisha popote

    Jibu

    Chelsea inahitaji Golikipa kama huyu kuchukua nafasi ya Kepa Arrizabaraga anayevujisha magoli langoni#meridianbettz

    Jibu

    Safari njema

    Jibu

    Bora aende zake atapata namba langoni

    Jibu

    Kila la kheri Bravo huko uwendako

    Jibu

    Kambi popote pale bravo

    Jibu

    Ni kipa mzur

    Jibu

    Acha Abadili Upepo tu

    Jibu

Acha ujumbe