Cavani Kubaki Manchester Baada Uruguay Kufuta Wito Wake

Edinson Cavani atabaki Manchester United wakati wa mapumziko ya kimataifa baada ya Uruguay kutangaza uamuzi wao wa kufuta wito wake kwaajili ya michezo ya kufuzu Kombe la Dunia lijalo.
Cavani Kubaki Manchester Baada Uruguay Kufuta Wito Wake
Edinson Cavani

Klabu zote 20 katika Premier Leageu zilikubaliana kwa kauli moja wiki iliyopita kutowachilia wachezaji kwa mechi za kimataifa kama wakipangwa katika ‘orodha nyekundu’ ya Uingereza.

Wachezaji wengi wa Amerika Kusini wameripotiwa kwenye orodha hiyo ya wasafiri wa coronavirus, ikimaanisha kuwa wachezaji wowote ambao wataamua kuichezea nchi zao watahitajika kuingia katika karantini kwa siku 10 baada ya kurudi England.

Cavani Kubaki Manchester Baada Uruguay Kufuta Wito Wake

Uruguay sasa imeondoa rasmi wito wao kwa Cavani kuungana na timu ya taifa, ikimaanisha ataendelea na mazoezi ya kawaida na Mashetani Wekundu katika wiki mbili zijazo badala ya kusafiri kwenda Amerika Kusini.

Taarifa kutoka Chama cha Soka cha Uruguay inasoma: “Kulingana na hali ambayo imetokea kwa wachezaji kutoka England, Chama cha Soka cha Uruguay kimeamua kusitisha wito wa Edinson Cavani.”


BADILI KILA KITU KWA SARAFU MOJA TU!

Unaweza kutengeneza faida kubwa huku ukiwa unaifurahia safari kabambe ya wacheza sarakasi kupitia sloti mpya ya Circus Fever Delux kupitia Kasino ya Meridianbet pekee Dau lako linaweza kukupa pesa maradufu kupitia kete au sarafu.

CHEZA SASA

Acha ujumbe