Mchezaji wa timu ya taifa ya Argentina Rodrigo De Paul amekasirishwa na unyanyasaji waliyoupata wakati walipokuwa Calama siku ya Alhamisi kumenyana na wenyeji Chile mchezo wa kufuzu kombe la Dunia.

Kiungo huyo alibainisha kwamba wenyeji hawakuwaruhusu hata kwenda msalani mara baada ya kushuka kwenye ndege yao.

Pamoja na chanamoto zote walizopata Argentina bado iliibuka na ushindi 2-1 magoli yaliwekwa kimiani na Angel Di maria na Lautaro Martinez. The Albiceleste inashika nafasi ya pili CONMEBOL na tayari wamefuzu kushiriki kombe la Dunia 2022.

“Hawakuturuhusu hata kwenda chooni tuliposhuka kwenye ndege,” De Paul aliwaambia wanahabari. “Walikata viyoyozi vyetu, hatukuwa na maji na walipiga ving’ora wakati wote wa kukaa.

“Sisemi ni sawa au si sawa, lakini, kama Muargentina, kila timu inayekuja nchini mwangu, lazima tuifanye ijisikie vizuri iwezekanavyo na lazima tushinde kwenye uwanja wa kuchezea inapostahili.”

Argentina ilipata ushindi ugenini licha ya kukosekana kwa kocha mkuu Lionel Scaloni sababu ya kuwa na maambukizi ya COVID-19 na nahodha wa timu hiyo Lionel Messi ambaye amepona hivi majuzi.


VUNA MKWANJA NA KENO

Dakika tano pekee zinakutosha kuwa mmoja wa washindi wa mkwanja mrefu ndani ya kasino pendwa ya meridianbettz katika sloti maridhawa ya KENO, moja ya michezo inayoipa thamani dau lako.

tetesi, Tetesi za Soka barani Ulaya., Meridianbet

CHEZA HAPA

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa