Díaz na James Waongoza Kikosi cha Colombia Kombe la Dunia 2026

Timu ya taifa ya Colombia imetangaza rasmi kikosi chake cha mwisho cha wachezaji 26 kitakachoshiriki michuano ya Kombe la Dunia 2026 itakayofanyika katika mataifa ya Marekani, Mexico na Canada. Kikosi hicho kimetangazwa usiku wa kuamkia leo Jumanne Mei 26, 2026 na kocha mkuu wa Colombia Néstor Lorenzo.

Díaz na James Waongoza Kikosi cha Colombia Kombe la Dunia 2026Miongoni mwa majina makubwa yaliyojumuishwa kwenye kikosi hicho ni mshambuliaji wa Colombia Luis Díaz ambaye anatajwa kuwa mmoja wa silaha muhimu za timu hiyo kuelekea mashindano hayo makubwa duniani. Díaz ameendelea kuwa tegemeo kubwa kutokana na kasi, uwezo wa kufunga pamoja na uzoefu wake katika soka la kimataifa.

Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa

Aidha, kiungo mshambuliaji mkongwe James Rodríguez pia amerejea katika kikosi hicho huku akitarajiwa kuongeza ubunifu na uzoefu mkubwa ndani ya safu ya kiungo. James, ambaye aliwahi kung’ara katika klabu za Real Madrid na Bayern Munich, anaendelea kuwa mmoja wa wachezaji muhimu wa Colombia katika mashindano ya kimataifa.

Díaz na James Waongoza Kikosi cha Colombia Kombe la Dunia 2026Akizungumza baada ya kutangaza kikosi hicho, Lorenzo alisema ana imani kubwa na wachezaji aliowachagua kuelekea Kombe la Dunia 2026. “Tumeunda kikosi chenye uwiano wa vijana wenye njaa ya mafanikio pamoja na wachezaji wenye uzoefu mkubwa wa mashindano ya kimataifa,” alisema kocha huyo wa Colombia.

Díaz na James Waongoza Kikosi cha Colombia Kombe la Dunia 2026Colombia inatarajia kufanya vizuri katika michuano hiyo huku mashabiki wengi wakiamini kuwa mchanganyiko wa vipaji vya vijana pamoja na uzoefu wa nyota kama Díaz na James unaweza kuipa timu hiyo nafasi kubwa ya kufanya vizuri katika Kombe la Dunia 2026.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.