Ijumaa ya tarehe 1 mwezi Aprili itafanyika droo rasmi ya michuano ya Kombe la Dunia 2022 katika nchi Qatar ambayo ndiyo wenyeji wa michuano hiyo.
Timu 15 kati ya 32 tayari zimefuzu wakiwemo wenyeji Qatar, Kutoka Ulaya, mabingwa wa zamani Ujerumani, Uhispania, Uingereza na Ufaransa tayari wameshakata tiketi zao za kwenda Qatar pamoja na Uholanzi, Croatia, Serbia, Uswisi na timu nambari 1 duniani, Ubelgiji.
Mabingwa wa zamani pia wamefuzu kutoka Amerika Kusini Brazil na Argentina tayari wamekata kibali cha kwenda Uarabuni.
Kutoka Asia, Iran na Korea Kusini pia watakuwa wakielekea Qatar.Mechi nyingine za kuufuzu zitaendelea kote ulimwenguni tarehe 24 Machi.
Tarehe na mahali droo ya Kombe la Dunia la FIFA itakapo chezeshwa
FIFA ilitangaza kwamba droo itafanyika siku ya Ijumaa ya tarehe 1 mwezi wa nne katika Kituo cha Maonyesho na Mikutano cha Doha (DECC) Sherehe hizo zitahudhuriwa na wageni waalikwa 2,000.
Michuano ya Kombe la Dunia itaanza kutimua vumbi tarehe 21 mwezi Novemba katika uwanja wa Al Bayt Stadium na kufikia tamati Disemba 18 katika uwanja wa Lusail Stadium.
Mchongo mpya mjini ni Shindano la Evoplay Spring Aweking katika kasino maridhawa za meridianbettz. Pata mgao wako wa TSh 25,000,000 katika michezo kibao ya kasino na sloti ziliyochaguliwa kushiriki.