Huenda Urusi ikawekewa vikwazo vya kuandaa mechi za mtoano kuelekea mashindano ya kombe la Dunia kufuatia nchi hiyo kufanya kuishambulia nchi jirani ya Ukrane.

Mechi za mchujo za Kombe la Dunia zimetiwa shaka baada ya Poland, Sweden na Jamhuri ya Czech kutoa taarifa ya pamoja zikisema hazitasafiri kwenda Urusi kwa mechi.

Poland, Sweden na Jamhuri ya Czech zote ziko katika ‘njia’ moja ya mchujo na Urusi, huku Poland ikitarajiwa kumenyana na taifa la Vladimir Putin katika moja ya nusu fainali ya Njia B.

Taarifa ya pamoja iliyotolewa na mataifa yote matatu imelaani kitendo cha Putin kuivamia Ukraine na kuamuru kwamba mechi za mchujo zisifanyike nchini Urusi.

Ilisomeka hivi: “Mashirikisho ya soka ya Poland, Uswidi na Jamhuri ya Czech yanalaani vikali uchokozi wa Urusi dhidi ya Ukraine. Kwa kuzingatia hali ya sasa, Chama cha Soka cha Poland (PZPN), Svenska Fotbollförbundet (SvFF) na Fotbalová asociace České republiky (FAČR) kueleza msimamo thabiti uliopangwa kufanyika Machi 24 na 29 mwaka huu. Mechi za mchujo kwa Kombe la Dunia nchini Qatar hazipaswi kufanyika katika Shirikisho la Urusi.

FIFA ilitoa wito “Vurugu kamwe si suluhu na FIFA inatoa wito kwa pande zote kurejesha amani kwa njia ya mazungumzo yenye kujenga. FIFA pia inaendelea kuonesha mshikamano kwa watu walioathirika na mzozo huu.


SHINDA IPHONE 12 NA KASINO YA AVIATOR

Meridianbettz na Aviator wanakupa mchongo wa kuibuka na iPhone 12 katika kasino ya Aviator itakayodumu kwa siku 7. Kuwa rubani wa Aviator na ujishindie!

tetesi, Tetesi za Soka Barani Ulaya., Meridianbet

SOMA ZAIDI HAPA

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa