Griezmann Amsifia Messi Kuwa ni "Ligendi."

Fowadi wa Barcelona Antoine Griezmann alimtaja Lionel Messi kama “Legend” baada ya nahodha huyo mashuhuri kutawala vichwa vya habari siku ya Jumapili.

Griezmann Amsifia Messi Kuwa ni "Ligendi."

Messi alianza kufunga kwa mpira wa adhabu dakika ya 20 na lilikuwa bao lake la 650 kwa Barca – kabla ya bao la Jordi Alba la kujifunga na kufanya ubao usomeke 1-1, ingawa Griezmann alifunga goli la pili na la ushindi kwa Barca dhidi ya Athletic Bilabao dakika 16 kabla ya kipyenga cha mwisho.

Baada ya gazeti la El Mundo kudai mkataba ambao Messi alisaini Camp Nou mwaka 2017 – ambao unamalizika mwishoni mwa msimu – una thamani ya zaidi ya milioni 555, Griezmann aliulizwa juu ya thamani ya mtu huyo wa miaka 33.

“Tunafurahi na Messi, ni legend (gwiji),” Griezmann alimwambia Movistar.

“Tunatumahi tunaweza kuendelea kufurahiya naye na anaweza kuendelea kutusaidia kushinda.”

Messi – anayetajwa kuondoka Barca huku akiwa na uhusiano mzuri na Paris Saint-Germain na Manchester City – amefunga mabao mawili ya moja kwa moja kutoka kwa majaribio yake manne ya mwisho kwa Barcelona kwenye mashindano yote, baada ya kufunga moja tu kutoka kwa majaribio 62 ya awali.

Kati ya mabao 650 ya Messi kwa Barcelona, ​​49 kati yao yamekuwa ni ya free-kick na 38 kati ya hayo amefunga katika LaLiga.

Messi ana mabao 12 na assist mbili kwenye ligi hiyo kwa Barca, ambao wako nafasi ya pili na alama 10 nyuma ya viongozi Atletico Madrid.


TUNGENEZA FAIDA KUPITIA KASINO YA MERIDIANBET

Neptune’s Richies ni mchezo Unaokupa pesa chap chap huku ukiwa unaburudika kupitia Kasino ya Mtandaoni ndani ya Meridianbet.

Neptune's-Riches_Casino-Post_30-January

Cheza hapa

11 Komentara

    Messi baba lao

    Jibu

    Ni kweli kabisaa messi lazima apewe sifa

    Jibu

    Messi asaivi analudi kivingine

    Jibu

    Messi ni balaaa

    Jibu

    Griezmann yupo sahihi Messi jembe

    Jibu

    Vizuri Messi mtu mbaya

    Jibu

    Messi ni legend kweli kabisa

    Jibu

    Anastahir pongez

    Jibu

    gud

    Jibu

    Safi

    Jibu

    Mie kwangu ni CR7

    Jibu

Acha ujumbe