Guardiola Ajivunia Rekodi ya Ushindi wa 15 Mfululizo.

Pep Guardiola amelezea furaha yake baada ya Manchester City kuweka historia kwa kufunga Swansea City bao 3-1 na kusonga mpaka hatua ya robo fainali ya FA Cup.

Guardiola Ajivunia Rekodi ya Ushindi wa 15 Mfululizo.
Wachezaji wa Man City wakipongezana baada ya kufunga goli.

Mabingwa na viongozi wa Premier League waliifunga timu ya Championship katika dimba la Liberty Stadium na kukamilisha idadi ya kushinda mechi 15 mfululizo na kuweka rekodi kwa hiyo katika timu hiyo ya EPL.

Kyle Walker alifunga goli la ufunguzi katika kipindi cha kwanza kabla ya Raheem Sterling kufunga goli lake la 12 kwa msimu huu mapema mwa kipindi cha pili na goli la tatu liliwekwa kimiani na Gabriel Jesus dakika chache baadaye.

Morgan Whittaker alifunga goli la kufutia machozi kwa upande wa Swansea City baada ya kupata kiungo wa Hispania Rodri kutolewa nje kwa majerha ambayo Guardiola amesema siyo kubwa sana.

Aliulizwa kuhusu rekodi mpya aliyoweka bosi huyo wa zamani wa Barcelona na Bayern Munich alisema: ” Huu ni ujumbe kwetu sisi wenyewe, tulikuja kushinda hicho ndiyo kitu cha umuhimu.

“Hatuwezi kukataa jinsi tunavyojisikia na kujivunia tulikuwa tunahitaji kuvunja rekodi hii kwa muda mrefu rekodi zipo kwaajili ya kuvunjwa.

“Siyo rahisi kwa soka la kisasa kushinda katika michezo 15 mfululizo tunajivunia na kufurahia na klabu yetu.

Guardiola atakuwa na tumaini la kuongeza point katika Premier League siku ya Jumamosi pale watakapo kabiliana na Tottenham katika dimba la Etihad Stadium.


TENGENEZA MKWANJA UKIWA NA MERIDIANBET 

Unaweza kuvuna mkwanja mrefu kadiri uwezavyo kupitia mchezo wa Gold n Rocks kwenye  kasino ya mtandaoni ya Meridianbet. Ni rahisi! Vigezo na masharti, kuzingatiwa.

SOMA ZAIDI

14 Komentara

    Guardiola ndiye kocha bora duniani kwa sasa. Ni rekodi inayovutia sana

    Jibu

    Hongera sana

    Jibu

    Nachompendea guardiola hanaga papara

    Jibu

    Hongera yao

    Jibu

    Guardiola anajua kuiongoza sana klabu ya man city ndie kocha bora zaidi vilabu vyote

    Jibu

    Guadiola ni kocha mzuri sana

    Jibu

    Hongera sana

    Jibu

    Pep mida yake ya kutawala

    Jibu

    Pep yuko vizur

    Jibu

    Pep yupo makini

    Jibu

    Hongera sana

    Jibu

    Hongera sana

    Jibu

    Namkubal

    Jibu

    Amerudi kwa kishindo

    Jibu

Acha ujumbe