Pep Guardiola alikosa nafasi kubwa ya kushinda taji lake la tatu la Ligi ya Mabingwa Ulaya huko Estadio do Dragao Jumamosi dhidi ya Chelsea. Kikosi cha Thomas Tuchel kiliipiga Sky Blues kwa mara ya tatu katika mashindano matatu tofauti katika kipindi cha mwezi mmoja tu.
Guardiola Ameshindwa Kufikia Malengo ya Kushinda UCL
Mabingwa Wapya wa Ligi ya Mabingwa 2021 Chelsea

Tangu kuteuliwa kwa Guardiola mwaka 2016, Manchester City wametawala soka la England, wakiwa wameshinda mataji matatu ya Ligi Kuu, mataji manne ya Kombe la Carabao, Kombe moja la FA na Ngao mbili za Jamii.

“Tulishindana vizuri sana,” alisema Guardiola baada ya fainali.

“Ilikuwa mara yetu ya kwanza kufika hapa. Lazima tujiandae kurudi siku moja.”

Mwalimu huyo wa Kikatalani aliifikisha Manchester City fainali yao ya kwanza kabisa ya Ligi ya Mabingwa. Baada ya misimu michache ya kuondolewa kwenye hatua ya robo fainali, Sky Blues iliwatoa Borussia Dortmund na Paris Saint-Germain wakielekea fainali ya mwaka huu.

Lakini, katika fainali walishindwa kuifunga Chelsea ambao walipata ushindi uliostahili wa 1-0 shukrani kwa bao la Kai Havertz katika kipindi cha kwanza.

Katika misimu mitano ya Guardiola klabuni, Manchester City wametumia euro milioni 938 kusajili na wameingiza euro 315m kutoka kwa mauzo.

Uwekezaji wa jumla wa euro 623m ulisababisha timu hiyo kushinda mataji 10, lakini Sky Blues hawajafanikiwa kufikia lengo lao la kwanza katika kushinda Ligi ya Mabingwa.


MAANA KAMILI YA USHINDI KATIKA KASINO ZA MERIDIANBETI NI PAMOJA NA MCHEZO WA PANDA PANDA.

Hii ndiyo burudani yenye ushindi! Ingia kwenye kasino ya Meridianbet kufukuzia ushindi huu. Cheza sasa Panda Panda na uwe moja ya washindi na Mabingwa.

Gomes, Gomes : Sitafanya Usajili wa Kutisha., Meridianbet

CHEZA HAPA

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa