Hazard Anataka Kucheza kwa Miaka Mitano Mingine.

Nyota wa Real Madrid Eden Hazard amesema kwamba anataka kuendelea kucheza kwa muda usiopungua miaka mitano mingine kati ya sita na mshambuliaji huyo alisisitiza kwamba kupata majeraha siyo mwisho wa dunia hali yakuwa amekuwa na changamoto ya kuwa fit huko Bernabeu.

Hazard Anataka Kucheza kwa Miaka Mitano Mingine.

Hazard aliondoka Chelsea na kutua Madrid kwa dau la €100m mwaka 2019 lakini tangu aanze kucheza ndani ya Uhispania amekuwa akikabiliwa na tatizo la majeraha ya mara kwa mara.

Mchezaji huyo wa miaka 30 ambaye anajiandaa kukosa ” wiki mbili au tau” kutokana na kupata tatizo la misuli katika mguu wake wa kushoto, ameanza katika michezo 20 katika LaLiga sita kati ya hiyo ilikuwa ni ya msimu huuna amefanikiwa kufunga mabao matatu pekee.

Hazard ameshindwa kumaliza dakika zote 90 kwenye mchezo wowote wa Madrid msimu 2020-21 katika mashindano yote, lakini Mbeligiji huyo bado ana mawazo chanya juu ya kinachoendelea katika soka lake.

“Bado ninatumaini la kucheza kwa muda mrefu kadri nitavyokuwa sawa na nimekuwa nikijaribu kujifurahisha mimi mwenyewe ndani ya uwanja,” aliiambia On The Front Foot.

“Linapokuja suala la kumaliza soka langu naweza kuangalia nyuma mafanikio niliyopata, lakini kipaumbele chnagu sasa ni kucheza vizuri na kufurahia mpira wa miguu.

“Nimefikisha miaka 30 sasa kama mwili wangu utakuwa sawa nitumaini langu naweza kuendelea kucheza kwa kipindi kisicho pungua miaka mitano au sita.


TENGENEZA MKWANJA UKIWA NA MERIDIANBET 

Unaweza kuvuna mkwanja mrefu kadiri uwezavyo kupitia mchezo wa Gold n Rocks kwenye  kasino ya mtandaoni ya Meridianbet. Ni rahisi! Vigezo na masharti, kuzingatiwa.

SOMA ZAIDI

14 Komentara

    Hazard yupo sahihi bado yupo fiti kuendelea kutumikia klabu yake kwa miaka mitano mingine

    Jibu

    Kama bado yupo na nguvu anaweza akaendelea tu

    Jibu

    Kama uwezo anao aendelee tu

    Jibu

    Hazard yupo sahihi

    Jibu

    Kama bado Yuko vizuri aendelee

    Jibu

    Nice update

    Jibu

    Pancha ya Hazard inamnyima raha sana

    Jibu

    Hazard yupo vizuri

    Jibu

    Good news

    Jibu

    Mchango wako Chelsea hautasahaulika, lakini mambo yamekuwa magumu mno kwa tangua atue Real Madrid

    Jibu

    Uwezo unaruhusu

    Jibu

    Nice

    Jibu

    Hazard aendelee kujituma tu

    Jibu

    Ataweza kweli

    Jibu

Acha ujumbe