Zlatan Ibrahimovic alidondosha machozi wakati akihojiwa na vyombo vya habari siku ya Jumatatu baada ya kuelezea kurejea kwake katika timu ya taifa ya Sweden amesema haijawa rahisi kwa familia yake.

Ibrahimovic Amwaga Machozi Kuiacha Familia Yake.

Straika wa Milan ameitwa tena katika kikosi cha timu ya Taifa cha Janne Andersson kwa mwezi huu kwaajili ya michezo ya kufuzu kushiriki Kombe la Dunia kwa michezo dhidi ya Kosovo na Georgia pamoja na mchezo wa kirafiki.

Alikuwa akisherehekea kuitwa kwake kwa mara ya kwanza katika timu ya taifa baada ya kupita miaka miaka mitano kwa kuweka post ya picha katiak akaunti yake ya Twitter na ujumbe uliyosomeka: “Kurejea kwa mungu.”

Ibrahimovic ambaye atafikisha umri wa miaka 40 mwezi Oktoba ndiyo mfungaji wa muda wote wa Sweden akiwa na mabao 62 na magoli yake ya mwisho alifunga kwenye mchezo dhidi ya Denmark mwaka 2015.

Akiongea na vyombo vya habari siku ya Jumatatu alikuwa ni mtu mwenye hisia akielezea jinsi ilivyokuwa ngumu kuicha familia yake na kujiunga na timu ya Taifa.

“Nina mtoto wangu wa kiume ambaye kiukweli alikuwa analia nilipo muacha.Lakini sawa….,” alisema kabla ya kuacha kububujikwa na machozi.

“Hili jambo la la kwenda mbali na familia yangu siyo jambo rahisi, kama una watoto wawili ambao wanalia kila wakati unapo waacha, ni ngumu kidogo, mimi ni binadamu ingawa ni Superman.


Maana Kamili ya Ushindi Katika Kasino za Meridianbeti ni Pamoja na Mchezo wa Tropical Wild.

Hii ndiyo burudani yenye ushindi! Ingia kwenye kasino ya Meridianbet kufukuzia ushindi huu. Cheza sasa Tropical Wild na uwe moja ya washindi na Mabingwa.

Ibrahimovic, Ibrahimovic Amwaga Machozi Kuiacha Familia Yake., Meridianbet

CHEZA HAPA

7 MAONI

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa