Nyota wa Milan Zlatan Ibrahimovic amemtaja gwiji wa Brazil Ronaldo kama “mchezaji bora katika historia”.
Ibrahimovic: Ni Ronaldo de Lima Mchezaji Bora wa Historia
Ronaldo de Lima.

Ibrahimovic alielezea kuvutiwa na mshindi wa Kombe la Dunia kabla ya Mechi ya Europa League na Red Star Belgrade Alhamisi usiku, wakati akimweka mbele ya wachezaji wakubwa wa siku hizi kama Lionel Messi na Cristiano Ronaldo katika orodha ya wakati wote ya wachezaji bora.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 39 anafikiria Ronaldo Nazario, ambaye alichochea Brazil kutwaa Kombe la Dunia mwaka 2002, aliupita mchezo huo na talanta zake za kipekee na bado anajulikana kama fundi wa soka hadi leo.

Ibrahimovic: Ni Ronaldo de Lima Mchezaji Bora wa Historia
Ibrahimovic akiwa na Ronaldo

Zlatan aliiambia Discovery Plus: “Sihitaji kumuelezea Ronaldo, ‘The Phenomenon’.

“Daima nasema kuna wachezaji wanaocheza soka, na wachezaji ambao ni soka. Kwangu, Ronaldo ndio mchezo. Unapomtazama akicheza, kila mtu alitaka kucheza kama yeye na kuwa kama yeye.

Ronaldo alianza kucheza soka la kulipwa nchini mwake na Cruzeiro mwaka 1993, na akaendelea PSV, Barcelona, ​​Inter, Real Madrid, Milan na Corinthians.

Fowadi huyo wa Brazil alifunga mabao 296 katika mechi 452 kwa jumla, wakati pia alishinda tuzo tatu za Mchezaji Bora wa Dunia wa FIFA na mbili za Ballons d’Or – ya kwanza ambayo ilimwona akiingia kwenye vitabu vya rekodi kama mshindi mchanga zaidi wa tuzo hiyo akiwa na miaka 21.


TENGENEZA FAIDA KATIKA SLOTI PENDWA HAPA MERIDIANBET

BusttheBank ni sloti inayokupa Mkwanja wa kutosha. Ndio, hii ni sloti inayokupa faida ya hadi mara kibao ya dau lako. Ni Meridianbettz pekee utakapoweza kupata burudani hii.

Ibrahimovic, Ibrahimovic: Ni Ronaldo de Lima Mchezaji Bora wa Historia, Meridianbet

CHEZA HAPA

8 MAONI

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa