Ibrahimovic: Nitacheza Mpaka Nione Mkali Zaidi Yangu

Zlatan Ibrahimovic hajawahi kuishiwa vioja safari hii amekuja na madai kwamba atastaafu kucheza soka kama akiona mchezaji bora kuliko yeye.

Zlatan ambaye amefikisha umri wa miaka 40 anaichezea klabu ya AC Milan ikiwa ni awamu ya pili akitokea LA Galaxy ya MLS mwaka 2020 akifanikiwa kufunga mabao 33 katika michezo 55.

“Historia bado inaandikwa, sijapanga kuacha, ngoja tusubiri tuone nini kitatokea,” Ibrahimovic aliiambia UEFA.com

“Sitaki kuja kujutia kwanini niliacha kucheza na taka kucheza vile ninavyoweza, Uhalisia ni kwamba nitacheza mpaka nitakapoona mchezji bora kuliko mimi hivyo naendelea kucheza.

Licha kucheza mechi 18 lakini bado Ibra ndiyo mfungaji bora wa Milan msimu huu akiwa na Rafael Leao na Olivier Giroud  wote wakiwa na mabao nane.


3500 NI YAKO UKIJIUNGA TU MERIDIANBET!

Una nafasi ya kupata bonasi ya shilingi 3500 kwa ajili ya kuanza safari yako ya kasino ya mtandaoni ya Meridianbet.

Kubeti Poa - Bonasi Kubwa

Jisajili sasa

Acha ujumbe