Lionel Messi amepona jeraha goti na sasa yupo tayari kuwakabili Manchester City katika ligi ya Mabingwa siku ya Jumanne usiku kwenye mchezo wa Kundi A Paris Saint-Germain wakiwa katika uwanja wa nyumbani Parc des Princes.
Tangu asajiliwe kama mchezaji huru kutoka klabu ya Barcelona Messi hajafanikiwa kufunga katika mchezo wowotekatika michezo mitatu aliyocheza mpaka sasa, mashabiki kote ulimwenguni wataelekeza macho kwenye mtanange huo ili kushuhudia goli namba 1 kwa Lionel Messi kama akifanikiwa kuifungia PSG.
Swali lilopo sasa ni je atafanikiwa kumaliza ukame wa mabao dhidi timu ya kocha wake wa zamani Guardiola, kuelekea mchezo huo Pep alisema.
“Kwa kiwango hiki cha ubora sijui ni jinsi gani naweza kuwazuia.”
“Wapo vizuri sana vipaji hivi ni ngumu sana, unatakiwa kuwazuia vizuri bila kuwaruhusu kukimbia na mpira ni wachezaji wa kipekee, kibinafsi na pale wanapo unganika.
SPACE SPIN NA MERIDIANBET.
Ni Mabingwa pekee Meridianbet wanakupa nafasi ya kushinda zaidi na mchezo wa Space Spin katika kasino bomba za meridianbet. Ni wakati wa kufurahia na kutengeza mkwanja bila kuwaza.