Mshambuliaji wa Manchester City Gabriel Jesus amekataa kuwaambia maripota kuhusu hatima yake huko Etihad na anataka kuangazia kumaliza msimu huu kwanza.

Jesus Agoma Kuongea Kuhusu Hatima Yake Etihad

Mkataba wa Jesus utaacha kufanya kazi Juni 2023, lakini kuna taarifa kwamba anaweza kutoa nafasi kwa Haaland anayehitaji kusaini kutoka Borussia Dortmund.

Mabingwa watetezi wa EPL wamehusishwa mara kwa mara na mshambuliaji wa Norway Haaland, huku kipengele cha kutolewa kwa euro milioni 75 kinaripotiwa kuanza kutumika mwishoni mwa msimu huu.

Huku mazungumzo yakiendelea kuhusu mustakabali wa Jesus, ambaye anatajwa kuhitajika na Arsenal, mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 25, alitinga uwanjani dhidi ya Watford, akifumania nyavu mara nne na kutoa asisti ya bao lingine katika ushindi wa 5-1 Jumamosi.

Hilo lilimfanya kuwa mchezaji wa tano wa Brazil mwenye hat-trick kwenye Premier League, baada ya Afonso Alves, Robinho, Roberto Firmino na Lucas Moura, lakini pia alikuwa mchezaji wa kwanza kufunga mabao manne kwenye mechi moja.

Hata hivyo, mshambuliaji huyo wa zamani wa Palmeiras alikataa kuongelea kuhusu mustakabali wake na City huku kukiwa na maswali kama atasalia na kupigania nafasi yake endapo Haaland atatua Man City.

“Huu sio wakati wa kufikiria juu ya hili. Sasa ni wakati mzuri zaidi wa msimu. Nataka kufurahia, kuweka umakini kwenye timu yangu, na wachezaji wenzangu, kupigania Ligi Kuu.


TENGENEZA FAIDA NA ZEUS ANCIENT FORTUNES

Una Kila sababu ya kufurahia wiki yako na kutengeneza mwaka huu uwe wa faida zaidi katika kasino zetu za mtandaoni za meridianbettz. Mchezo wa Zeus Ancient Fortunes unakuongoza kutekeleza hilo.

tetesi, Tetesi za Soka Barani Ulaya., Meridianbet

CHEZA HAPA

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa