Juventus wameonywa na rais wa Shirikisho la Soka la Italia (FIGC) Gabriele Gravina kwamba wanakabiliwa na kufukuzwa kutoka Serie A kama hawatajiondoa katika Super League
Juventus Yanyoshewa Kidole na Shirikisho la Soka Italia
Vilabu ambavyo havija jitoa kwenye European Super League Barcelona, Real Madrid na Juventus

Miamba hao wa Italia, Real Madrid pamoja na Barcelona, ​​ni moja ya matajiri watatu kati ya 12 wa Ulaya ambao walisaini kujiunga kwenye ligi hio yenye utata.

Milan, Inter na Atletico Madrid walijiondoa kwenye mashindano muda mfupi baada ya kutangazwa mwezi uliopita, kufuatia uongozi wa vilabu “vikubwa sita” vya England, lakini Juve bado hawajayakataa mashindano hayo ambayo yanashinikiza mageuzi katika mpira wa miguu wa Ulaya.

UEFA wiki iliyopita ilizionya vilabu vitatu vya waasi kwamba vina hatari ya kuzuiliwa kwa sababu ya msimamo wao usioyumba.

Lakini, Juve ilitoa taarifa ya pamoja ikielezea maonyo hayo kama “hayavumiliki” na “hayakubaliki”, ikisema kuwa mapinduzi ya muundo ni lazima yafanyike kwa faida ya mchezo.

Mkuu wa FIGC Gravina ana matumaini Bianconeri watajiweka mbali na mashindano mapya yaliyopendekezwa, la sivyo watakabiliwa na kufukuzwa kwenye ligi kuu ya Italia.

“Sote tumechoka kidogo na vita hii ya kuvuta nikuvute kati ya UEFA na vilabu hivi vitatu. Natumai kuweza kupatanisha kati ya Juventus na UEFA.

“Sio nzuri kwa mpira wa miguu wa kimataifa, mpira wa miguu wa Italia, Juventus. Tayari tumesema kuwa chama cha mpira wa miguu kinaheshimu sheria.

Mwenyekiti wa Juventus Andrea Agnelli ametajwa kuhusika kwa kuwa na jukumu katika kuandaa Super League.


PESA IPO HAPA KATIKA KASINO YA LUCKY LUCKY.

Hii ndiyo burudani yenye ushindi! Ingia kwenye kasino ya Meridianbet kufukuzia ushindi huu. Cheza sasa Lucky Lucky na uwe moja ya washindi na Mabingwa.

Juventus, Juventus Yanyoshewa Kidole na Shirikisho la Soka Italia, Meridianbet

CHEZA HAPA

5 MAONI

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa