Kadi nyekundu ya moja kwa moja ya Granit Xhaka dhidi ya Liverpool katika sare ya 0-0 kwenye Kombe la Carabao Alhamisi imeiweka Arsenal kwenye wakati mgumu kwa mechi yao ya Ligi Kuu ya Uingereza dhidi ya Tottenham wikendi hii.
Xhaka alimchzea madhambi Diogo Jota katika dakika ya 24 ya mchezo wa nusu fainali ya kwanza ya Carabao Cup na inakuwa ni kadi yake ya tano tangu 2016-17.
Kwa matokeo hayo, ataungana na Thomas Partey (Afcon), Mohamed Elneny (Afcon), Martin Odegaard (mgonjwa) na Emile Smith Rowe (majeruhi) kuwa miongoni mwa wachezaji wa Gunners ambao huenda wakakosekana kwenye mechi muhimu la derby Jumapili.
“Kulingana na namba tulizonazo, hatuna kiungo wa kati, inakuwa ngumu sana, kwa sababu chochote tunachofanya sio kawaida,” meneja Mikel Arteta aliambia Sky Sports. “Motisha ya ziada ya kucheza derby huko Tottenham Jumapili huleta nguvu wakati huna. Hakuna visingizio, lazima tucheze.”
Akisisitiza juu ya uwezo wa timu yake kuokoa sare dhidi ya Liverpool wakati akiwa chini, alisema: “Tunafurahia hali hiyo. Wachezaji walionyesha mapambano makubwa, dhamira, undugu. Uliona hisia, hatukukata tamaa. Sifa ziendee kwa vijana.
Ni muda wako kujiachia na mchezo maridhawa wa Almighty Aztec katika kasino bomba za meridianbettz. Nafasi ya kutengeneza mkwanja iko mikononi mwako kazi ni kwako.
CHEZA HAPA