Nyota wa Harambee Stars Francis Kahata anaamini kwa sasa Ligi kuu ya Tanzania Bara ni ligi bora kuliko ya Kenya maarufu kama Football Kenya Federation Premier League.
Kahata: Ligi ya Tanzania Ni Bora Kuliko ya Kenya.
Francis Kahata

Kiungo huyo mwenye kipaji amekuwa akicheza katika ligi ya Tanzania kwa misimu miwili mfululizo baada ya kujiunga na Simba akitokea klabu ya Gor Mahia. Amefunguka kwanini anaamini ligi ya ya Tanzania inakuwa kwa kasi sana.

“Ligi kuu Tanzania bara inaendelea kwa kasi ,” Kahata alielezea.

“Tulikuwa na ligi bora nyumbani Kenya, lakini tangu wadhamini wajiondoe kuidhamini ubora wa ligi umeshuaka sana.

“Hiyo ndiyo sababu kwanini wachezaji wengi mfano sisi tupo hapa kucheza soka, kuna wachezaji ambao wapo nyumbani ambao wanatutizama sisi tukiwa tunacheza hapa na wamatamani kuja hapa pia.”

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 29 alikuwa na maelezo mengi juu ya jinsi mabingwa mara 21 walivyoweza kuisadia kuitangaza ligi.

“Simba wamechukua nafasi kubwa sana katika kuiuza soka la Tanzania.Wamefanya hivyo kwa kushinda michezo mikubwa mfululizo,” Khata aliendelea.

Hivi karibuni Wekundu wa Msimbazi waliifunga Al Ahly katika michuano ya Caf Champions League katika dimba la Benjamin Mkapa Stadium na mchezaji raia wa msumbiji Luis Miquissone alifunga goli pekee na la ushindi kwa timu ya Simba.


Ni Muda wa Kuvuna Mkwanja na Jungle Jim and the Lost Sphinx

Hauihitaji kufikira mara mbili ni mchezo gani utakupatia mkwanja ndani ya kasino za Meridianbet. Jiunge sasa ufurahie Jungle Jim and the Lost Sphinx.

Tanzania, Kahata: Ligi ya Tanzania Ni Bora Kuliko ya Kenya., Meridianbet

  CHEZA HAPA

9 MAONI

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa