Koeman Kurithi Mikoba ya Van Gaal Baada ya World Cup

Kocha wa zamani wa Barcelona Ronald Koeman atarejea katika majukumu ya kuinoa timu yake ya taifa ya Uholanzi baada ya kumalizika kwa michuano ya kombe la Dunia 2022 nchini Qatar.

Koeman atachukua nafasi ya Louis van Gaal ambaye hivi majuzi alitangaza kuwa anapambana na saratani ya tezi dume licha ya kuwa changamoto hiyo Van Gaal bado ataendelea kuwa kocha wa Uholanzi katika michezo inayokuja ya kombe la Dunia.

Koeman aliondoka kwenye majukumu kama kcoha mkuu wa Uholanzi mwaka 2020 na kujiunga na klabu ya Barcelona na sasa anajiandaa kurejea baada ya kutimuliwa na Barca mwaka 2021.

“Ninatazamia ushirikiano mpya,” Koeman alisema. “Zaidi ya mwaka mmoja na nusu uliopita, hakika sikuiacha timu ya taifa ya Uholanzi kwa kutoridhishwa.

“Uwepo wangu ulikuwa mzuri, matokeo yalikuwa mazuri na uhusiano na wachezaji ulikuwa mzuri. Hivi karibuni tutaendelea kwenye njia hiyo, hilo ni hakika kwangu”


3500 NI YAKO UKIJIUNGA TU MERIDIANBET!

Una nafasi ya kupata bonasi ya shilingi 3500 kwa ajili ya kuanza safari yako ya kasino ya mtandaoni ya Meridianbet.

Kubeti Poa - Bonasi Kubwa

Jisajili sasa

 

Acha ujumbe