Kudela Akutana na Rungu la UEFA, Kamara Nje Mechi 3.

Mlinzi wa Slavia Prague Ondrej Kudela amefungiwa kutocheza mechi 10 kwa kumfanyia ubaguzi wa rangi Glen Kamara, lakini kiungo wa Rangers naye amefungiwa mechi tatu kutokana na kitendo chake cha kujibu kwa lugha mbaya.

Kudela Akutana na Rungu la UEFA, Kamara Nje Mechi 3.

Wawili hao walitofautiana mwishoni mwa mchezo wa pili Europa League hatua ya 16 bora huko Ibrox na Kamara alikasirishwa baada ya kufanyiwa kitendo cha kibaguzi na Kudela kabla ya wachezaji wa timu zote kuingilia kwenye mgogoro huo.

Uchunguzi wa UEFA sasa umeonesha kwamba Kudela alikuwa na hatia kwa ubaguzi na amefungiwa lakini Kamara atalazimika kukaa nje kwa michezo mitatu kwa kumtusi mchezaji mwingine.

Taarifa kutoka Shirikisho la mpira wa miguu la Ulaya limesema kwamba: Kwa uchunguzi wake wa Maadili na Nidhamu lilikuwa limeamua: “Kumuadhibisha mchezaji wa SK Slavia Praha, Ondrej Kudela kwa Mechi 10 za mashindano ya klabu na wawakilishi wa UEFA ambayo angestahili kucheza, kwa tabia ya kibaguzi. “

Na imesema adhabu hiyo itahusisha mchezo wa robo fainali ya Europa League dhidi ya Arsenal baada ya kuukosa mchezo wa kwanza kutokana na kufungiwa kutocheza.

Kamara alisema Kudela alimuita “f*cking Monkey” yaani “wewe Nyani” kuelekea mwishoni mwa mchezo ambao Slavia ilishinda kwa 2-0 dhidi ya Rangers wakitafuta tiketi ya kucheza 8 bora.


JILIPE KWA NAMBA ZAKO ZA BAHATI NA KENO

Kila mtu ana namba zake za bahati, Meridianbet tunatambua namba zinaweza kukufanya milionea leo. Jilipe kwa namba zako za bahati kila baada ya dakika tano.

CHEZA HAPA

3 Komentara

    Safi sana

    Jibu

    Inapendeza

    Jibu

    Sio kitu kizur kufanya ubaguzi

    Jibu

Acha ujumbe