Mshambuliaji wa timu ya Manchester City Sergio Kun Aguero, ameomba msamaha baada ya kupiga penati mbovu iliyowafanya wakose pointi kwenye mchezo wa Ligi kuu ya England dhidi ya Chelsea Fc
Mchezo huo ulichezwa juzi Jumamosi tarehe 7 Mei, 2021 katika uwanja wa nyumbani wa Manchester City Etihad, na kuchapwa mabao 2-1 na Chelsea. Jambo lililowafanya washindwe kutangazwa kuwa mabingwa wa Ligi kuu ya England.
Jana baada ya Manchester United kushinda dhidi ya Aston Villa umewafanya Manchester City kutotwaa ubingwa huo, hivyo wanakazi ya kusaka ushindi kwenye mechi zao zilizobaki.
Nyota wa timu hiyo Kun Aguero amesema:”Napenda kuomba msamaha kwa wachezaji wenzagu, viongozi pamoja na mashabiki wa soka kutokana na kukosa penalti ile.
“Yalikuwa ni maamuzi mabaya sana na napenda kuwahakikishia kuwa lawama zote zinanihusu mimi,“.
Kocha Mkuu wa timu hiyo ya Manchester City, Pep Guardiola amesema kuwa alimuambia nyota huyo awe makini hivyo hawezi kujua ni jambo gani ambalo lilimkuta.
Hii ndiyo burudani yenye ushindi! Ingia kwenye kasino ya Meridianbet kufukuzia ushindi huu. Cheza sasa Lucky Lucky na uwe moja ya washindi na Mabingwa.
duuh sio pw wamsamehe tuu
Asamehewe kwa kujua alichokosea
Wamsamehe tu kama katambua kosa lake
Wamsamehe tuu
Daah wamsamee tuu
Bahat mbay
Iyo ni mitihani katika michezo