Liverpool: Diaz Nje Mechi 10 kwa Majeraha

Mchezaji wa Liverpool Luis Diaz imebainika kuwa atakosa michezo takribani kumi ijayo, kutokana na jeraha la goti alilolipata kwenye mchezo kati ya Arsenal dhidi ya Liverpool.

Katika mchezo huo uliomalizika kwa Majogoo kuendeleza na jinamizi la matokeo mabaya, baada ya kupoteza kwa jumla ya magoli 3-2, magoli ya majogoo yakifungwa na Nunez, na Firmino huku kwa upande wa Arsenal yakifungwa na Martineli, na Saka alizama kambani mara mbili na kufanya ubao usomeke mpaka kipyenga cha mwisho, 3-2.

 

Liverpool: Diaz Nje Mechi 10 kwa Majeraha

Matokeo hayo yanaifanya Liverpool kufikisha jumla ya alama 10 na kushika nafasi ya 10 kwenye msimamo wa EPL, huku upande wa Arsenal wao wakiwa ndio vinara wa Ligi kwa alama 24 wakiwazidi Manchester City alama moja.

Liverpool: Diaz Nje Mechi 10 kwa Majeraha

Klopp anaendelea kukumbwa na tatizo la majeraha ambapo baadhi ya wachezaji wake tegemezi kama, Keita, Trent Alexander-Anold, Andy Robertson, Arthur Melo, Curtis Jones, na Alex Oxlade-Chamberlain

Acha ujumbe