Klabu ya Arsenal ipo kwenye windo la kuinasa saini ya kinda wa Kibrazil Marquinhos kutoka Sao Paulo hii ni kwa mujibu wa mwandishi maarufu wa nchini Brazil Jorge Nicolas ambaye aliiambia Yahoo! kwamba winga huyo tayari amefanya makubalinao binafsi na The Gunners.

Marquinhos ambaye ametimiza umri wa miaka 19 anaweza kuhama kutoka ligi ya Brazil mpaka Premier League akiwa na umri mdogo jambo ambalo halijazoeleka kwa vilabu vya england.

Marquinhos ni mchezaji mwenye kipaji cha kipekee ambaye anatumia kwa umahiri mguu wa kushoto na anauwezo wa kucheza eneo la kiungo. Alipenya katika kikosi cha wakubwa cha Sao Paulo mwaka 2021 wakati akiwa na miaka 18.

Na huenda Arsenal wakamtoa kwa mkopo msimu ujao na walenga kumpeleka katika ligi ya Hispania kwa hiyo usajili huu ni azina ya badaye kwa Arsenal.

Taarifa pia zinadai Arsenal wapo tayari kumsajili Gabriel Jesus kutoka Manchester City ambapo City wanataka kiasi cha £40-£50M na mazungumzo yataanza muda mfupi.


TENGENEZA FAIDA NA ZEUS ANCIENT FORTUNES

Una Kila sababu ya kufurahia wiki yako na kutengeneza mwaka huu uwe wa faida zaidi katika kasino zetu za mtandaoni za meridianbettz. Mchezo wa Zeus Ancient Fortunes unakuongoza kutekeleza hilo.

tetesi, Tetesi za Soka Barani Ulaya., Meridianbet

CHEZA HAPA

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa