Mashabiki wa Liverpool wanawageukia wamiliki wao wa Marekani, Fenway Sports Group, kwa kukosa uwekezaji baada ya kushindwa kwao na Leeds United.

Crysencio Summerville alifunga bao la ushindi dakika za lala salama wakati Leeds ilipowalaza na viatu Liverpool kwa kuwafunga nyumbani kwao Anfield bao 1-2 na kuongeza huzuni katika mwanzo wao mbaya wa msimu.

 

Mashabiki Liverpool Wamjia Juu Mmiliki wa Timu

Rodrigo alitangulia kuifungia timu ya Jesse Marsch baada ya kuukwamisha mpira wavuni baada ya makosa ya mlinzi Joe Gomez, lakini haikudumu kwani wenyeji walijibu Mohamed Salah alipomalizia mpira wa krosi kutoka kwa Andrew Robertson.

Summerville aliuchukua mpira kutoka kwa Patrick Bamford na kumpita kipa wa Reds Alisson Becker katika dakika za mwisho za mechi hiyo iliyochezwa Anfield.

 

Mashabiki Liverpool Wamjia Juu Mmiliki wa Timu

Fenway Sports Group (FSG) ilinunua Liverpool tena mwaka wa 2010 na kufurahia mafanikio mengi tangu kwa kushinda Ligi Kuu, Ligi ya Mabingwa, Kombe la Dunia la Vilabu la FIFA, UEFA Super Cup, Kombe la FA, Kombe la Ligi na Ngao ya Jamii.

Mashabiki, hata hivyo, wamefurika mitandao ya kijamii kuwageukia wamiliki wa klabu hiyo kutoka Marekani kwa kushindwa kuwekeza kwenye kikosi hicho ili kubaki miongoni mwa vinara wa Ligi Kuu ya Uingereza.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa