Jeraha la Ansu Fati ni gumu kujadilika, na mchezaji huyo na timu yake wamelinganisha muda wa kutokuwepo kwa wachezaji wengine ambao walikuwa na tatizo kama hilo, na wameamua kwamba anaweza kurejea baada ya siku 60.

Maskini Ansu Fati Nje Tena Siku 60

Wachezaji kadhaa wamekuwa na shida kama hii, huku Sergio Canales wa Real Betis akiwa ndiye mchezaji pekee aliyerejea mapema kuliko ilivyotarajiwa, na kuweza kushinda katika siku 42.

Wakati huohuo, nyota wa Real Madrid Rodrygo na Dani Carvajal wote walipata nafuu ndani ya wiki moja ya alama ya siku 60.

Umekuwa ni wakati mgumu kwa mshambuliaji huyo chipukizi, ambaye amekosa sehemu kubwa ya mwaka jana kutokana na majeraha.

Fati alikosa takribani miezi tisa kutokana na jeraha la goti kabla ya kurejea na kusumbuliwa na tatizo la misuli ya paja.

Kama Fati atarudi baada ya siku 60, atarejea siku moja tu kabla ya El Clasico, hivyo kurejea mapema kunaweza kuwa msaada mkubwa kwa Barca.


VUNA MKWANJA NA KENO

Dakika tano pekee zinakutosha kuwa mmoja wa washindi wa mkwanja mrefu ndani ya kasino pendwa ya meridianbettz katika sloti maridhawa ya KENO, moja ya michezo inayoipa thamani dau lako.

tetesi, Tetesi za Soka barani Ulaya., Meridianbet

CHEZA HAPA

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa