Nyota wa Paris Saint-Germain, Kylian Mbappe alifurahi baada ya kufunga bao lake la 100 la Ligue 1 mwishoni mwa wiki, ambalo alilielezea kama “hatua mpya kuelekea historia”.

Mbappe Afikisha Mabao 100 Katika Ligue 1

Mbappe alifunga bao la ufunguzi la PSG dakika 15 katika mchezo wao wa juu dhidi ya Lyon siku ya Jumapili usiku.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 22 aliweka wavuni tena katika kipindi cha pili kuongeza idadi ya mabao katika ligi ya Ufaransa wakati kikosi cha Mauricio Pochettino kilipoibuka na ushindi wa 4-2, na alionyesha njaa yake ya kuendelea na kufanikisha mambo makubwa zaidi baada ya filimbi ya mwisho.

“Ilikuwa siku nzuri kufunga bao langu la 100 kwenye Ligue 1,” Mbappe aliiambia Canal Plus. “Nilijua nilikuwa nimebakisha mabao mawili. Baada ya kumpa [mshambuliaji wa Nantes] Randal Kolo Muani bao wiki iliyopita, ilibidi nilipate!

“Ni hatua nyingine katika taaluma yangu, hatua nyingine kuelekea historia. Ndiyo kwanza kazi imeanza tu.”

Mbappe alianza taaluma yake huko Monaco mwaka 2015, na hakuchukua muda mrefu kufanya alama yake baada ya kuhitimu kwenye kikosi cha wakubwa.

Mfaransa huyo alifunga mabao 27 katika michezo 60 akiwa kwenye mavazi ya Stade Louis II, pamoja na 16 kwenye ligi wakati akiisaidia klabu kushinda taji hilo katika kampeni yake ya 2016-17.

PSG ilimshawishi Mbappe kwenda Parc des Princes mwishoni mwa msimu huo na tangu wakati huo amekua na muendelezo mzuri sana.


Maana Kamili ya Ushindi Katika Kasino za Meridianbeti ni Pamoja na Mchezo wa Tropical Wild.

Hii ndiyo burudani yenye ushindi! Ingia kwenye kasino ya Meridianbet kufukuzia ushindi huu. Cheza sasa Tropical Wild na uwe moja ya washindi na Mabingwa.

Mbappe, Mbappe Afikisha Mabao 100 Katika Ligue 1, Meridianbet

CHEZA HAPA

8 MAONI

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa