Kylian Mbappe amerejea Paris Saint-Germain kufuatia mapumziko baada ya Euro 2020 akiwa anaangalia kuanza maandalizi ya pre-season lakini hana mpango wa kuongeza mkataba mpya.
Anafurahia kurejea kwenye klabu yake kuelekea msimu mpya kama ilivyoonekana kwenye picha yake aliyoiweka kwenye akaunti yake akiwa na tabasamu kubwa wakati wa mazoezi huko Camp des Loges malengo yake ni kwaajili ya msimu unaokuja na utakuwa msimu wake wa mwisho na klabu hiyo.
Mkataba wake unatarajiwa kufika mwisho mwaka ujao majira ya joto na ingawa hataki kulazimisha kuondoka wakati huu wa dirisha la uhamisho, mpango wake ni kutoongeza muda wa kukaa Paris.
Wakati huohuo analengo la kufurahia msimu huu na klabu ya PSG, mahala ambapo anajihisi kupashukuru kwa kile alichokipata tangu aliposaini mwaka 2017.
Rais wa klabu Nasser Al-Khelaifi alitangaza katika msimu wa mwisho kwamba Mbappe siyo tu atasalia klabuni kwa msimu 2021-22 bali pia atasaini mkataba mpya.
Wakati huu PSG tayari imenasa saini za wachezaji kadhaa wakiwa kwenye ushawishi wa kumbakiza mkali huyo wa miaka 22 na Pogba huenda ikawa sajili inayofuata baada ya kumsajili Ramos, Achraf Hakimi Wijnaldum na Donnarumma.
Kasino ya Mayan Eagle inakukufanya kuwa bingwa wakati wowote unapoamua kuicheza. Utaburudika huku ukiendelea kutengeza mkwanja mrefu, jiunge sasa na uwe miongoni mwa mabingwa!!
Ernest
Hii ni habari nzuri kwa Real Madrid wanatakiwa kuweka Mkwanja Mezani