Mbappe: Usaliti Kumuondoa Psg

Uhusiano wa Kylian Mbappe na PSG umefikia ukingoni, kulingana na ripoti kutoka Ufaransa, kwa sababu anahisi kuwa amesalitiwa na klabu hiyo baada ya kuafiki mkataba mpya msimu huu.

Mshindi huyo wa Kombe la Dunia 2018 alifichua nia yake ya kutaka kuondoka kwenda Real Madrid, ambayo ilitoa ofa ya paundi milioni 154 kwa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 23, msimu wa joto kabla ya kuwakataa wababe hao wa Hispania kusaini mkataba mpya wa paundi 650,000 kwa wiki mjini Paris.

 

Mbappe: Usaliti Kumuondoa Psg

Mbappe aliahidiwa kuwa angekuwa na uhuru zaidi wa kucheza kwenye safu ya winga, jambo ambalo halijatimia kikamilifu hadi sasa msimu huu na kumfanya akose furaha.

Tangu wakati huo imefichuka kuwa uhusiano kati ya Mbappe na klabu hiyo kwa sasa upo kwenye hatua mbaya, si tu kutokana na nafasi, lakini ukweli kwamba mshambuliaji anahisi kusalitiwa na klabu hiyo miezi mitano tu baada ya kusaini mkataba mpya, kwa mujibu wa L’Equipe.

 

Mbappe: Usaliti Kumuondoa Psg

Ripoti hiyo inadokeza kwamba mabingwa hao wa Ligue 1 walikuwa wamemuahidi dirisha kubwa la uhamisho ikiwa ni pamoja na kuwasajili wachezaji kama Robert Lewandowski, Bernardo Silva na Milan Skriniar ili kuwasaidia hatimaye kushinda Ligi ya Mabingwa.

Mshauri wa masuala ya michezo Luis Campos aliletwa na kupewa jukumu la kusajili majina makubwa na kupanga kuondoka kwa Neymar, kwa hoja kwamba Mbappe na supastaa huyo wa Brazil wanacheza katika nafasi moja.

 

Mbappe: Usaliti Kumuondoa Psg

Mbappe amepunguza kiwango cha kutokuwa na furaha nchini Ufaransa mwanzoni mwa msimu mpya na amekashifu waziwazi mbinu za kocha Christophe Galtier na pia anaonekana kukosana na Neymar.

Acha ujumbe