Gundu inaendelea kwenda sambamba na Mason Mount katika uwanja wa Wembley amepoteza katika fainali sita zilizochezwa kwenye dimba hilo.

Mount Hana Bahati na Wembley Stadium Fainali 6?

Huenda ikamchukua muda kidogo kusahau fainali ya siku ya Jumamosi Chelsea dhidi ya Liverpool katika kuwania taji la FA Cup baada ya yeye kukosa penati na kupelekea Liver kuondoka na kombe la FA 2021-22.

Ilikuwa ni fainali ya sita katika miaka mitatu iliyopita na zote akiishia kuwa mshindi wa pili kwenye uwanja huo maarufu nchini Uingereza. Fainali ya kwanza alipoteza kipindi akiwa Derby County kwa mkopo walipokutana na Aston Villa na kupoteza kwa 2-1.

Fainali ya pili ilikuwa FA Cup 2020 ambapo Chelsea walipoteza kwa 2-1 dhidi ya Arsenal, Mzimu wa Wembley uliendelea kumtesa Mount katika fainali nyingine ya FA Cup 2021 The Blues walipoteza kwa 1-0 dhidi ya Leicester City.

Mount akiwa na timu ya taifa ya Uingereza walipoteza fainali ya Euro 2020 dhidi ya Italy kwenye mikwaju ya penalti katika uwanja huohuo wa Wembley.

Mwaka huu amepoteza fainali mbili dhidi ya Liverpool kwenye michuano ya Carabao Cup na FA Cup zote zikiwa ni kwenye mikwaju ya penati.

Kuna methali moja inasema “Asiye na bahati kamwe habahatiki” Mount anahitaji maombi ili aweze kunyanyua ndoo kwenye uwanja mshuhuri wa Uingereza Wembley Stadium?


TENGENEZA FAIDA NA ZEUS ANCIENT FORTUNES

Una Kila sababu ya kufurahia wiki yako na kutengeneza mwaka huu uwe wa faida zaidi katika kasino zetu za mtandaoni za meridianbettz. Mchezo wa Zeus Ancient Fortunes unakuongoza kutekeleza hilo.

tetesi, Tetesi za Soka Barani Ulaya., Meridianbet

CHEZA HAPA

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa