Mashabiki wa Yanga bado hawana furaha na timu yao na wala hawakubaliani na jinsi chama lao linavyotaabika mbele ya timu ndogo katika mechi zao za Ligi Kuu, lakini kiungo wao, Mukoko Tonombe naye ametia neno kwa mastaa wote akiwamo yeye kuwa wanastahili lawama hasa kama watashindwa kutimiza lengo la kubeba ubingwa.

“Sioni uhakika wa hilo naona tunazidi kujiweka katika nafasi ngumu kwenye malengo hayo (ya ubingwa), sio hatua nzuri kuendelea kuangusha pointi,tulipaswa kuendelea kushinda lakini hali haiko hivyo,” alisema Mukoko na kuongeza;
“Matokeo yetu yanazidi kutupunguza nguvu lakini yanatoa morali kwa tunaofukuzana nao hapo ndio ugumu unakuja.”
“Hatujaweza kucheza kwa ubora mkubwa tukiwa kama wachezaji wa Yanga, nawaonea huruma mashabiki na hata uongozi walitarajia makubwa lakini tumewaangusha,” alisema Mukoko na kuongeza;
.
“Sikuzote nimekuwa nikisema kwamba hii ni klabu kubwa unaposaini mkataba wa kuja hapa unatakiwa kuelewa unaingia katika klabu ambayo unatakiwa kupambana ishinde.”
Kila mtu ana namba zake za bahati, Meridianbet tunatambua namba zinaweza kukufanya milionea leo. Jilipe kwa namba zako za bahati kila baada ya dakika tano.
Adelta
Kwa sasa yanga wajipange upya ili waweze kuwa Bora zaidi msimu ujao
Venerose
Yanga wametuangusha kwa kweli msimu huu
Sarah
Yanga wameshuka kiwango
dorophina
Yanga walianza vizuri mwishoni wanabolonga vibaya
warda
Na bado wataumia